SOKO LA MDINI ULANGA LA KUSANYA MILIONI 396 NDANI YA MIEZI 5

  • Waziri wa Madini Doto Biteko amesema tangu kuanzishwa kwa soko la madini Ulanga wamenunua madini ya Tsh 396 milioni ndani ya miezi 5 mpaka sasa na kwamba awali kabla ya kuanzishwa kwa soko hilo walikuwa wanauza madini hayo kwa milioni 4 tu kwa miaka 5. “Kwa nini nisiseme naongea kwa takwimu? alisema Biteko.
  • Amesema hayo jana tarehe 1/2/2020 wilayani  Ulanga wakati wa ghafla ya kukata utepe na kukabidhi ofisi  na funguo za serikali za vijiji vitatu vya Nawenge, Kisewe na Mdindo, zilizojengwa na mwekezaji wa Mahenge Resources Ltd  katika hatua zake za awali kabla ya kuanza kuchimba madini ya graphite.
1-01
Waziri wa Madini Doto Biteko akihutubia wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo kabla ya zoezi la kukabiidhi funguo za ofisi za serikali za vijiji vitatu
  • “Madini yamechimbwa muda mrefu sana, lakini madini haya yalikuwa hayaachi alama kwenye jamii zetu, nafurahi kuona Mahenge Resources Ltd wanampango wenye kuweka alama kwa shughuli zao kwa jamii yetu. Mipango yao iko wazi juu ya maslai ya wananchi, nimemwagiza Mkuu wa wilaya Ngollo Malenya asimamie yale yote yaliyokubaliwa kwa ajili ya utekelezaji”. alisema Biteko.
  • Akikabidhi funguo za ofisi hizo kwa waziri wa madini, Mkurugenzi Mtendaji  wa  Mahenge Resources Ltd, John De Vries, wanafurahi kuungana na waziri ili wamkabidhi majengo ya serikali za vijiji vitatu. “Tupo teyari kwa ajili ya kutekeleza yale yote tuliyokubaliana” alisema Vries.
3-01
Mkurugenzi Mtendaji wa Mahenge Resources Ltd John De Vries akitoa hotuba yake kabla ya kukabidhi funguo za vijiji vitatu vya Nawenge, Kisewe na Mdindo wilayani Ulanga kwa Waziri wa Madini.
  • Kwa upande wake, Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga alimshukuru Waziri wa Madini kwa kufika kwake. Alisema madini ya Ulanga yamechimbwa muda mrefu lakini hayajatupa faida, awamu hii tunaona yameanza kutupa faida.
  • Mlinga alisema ni bora mtu akumbatie transformer ya umeme anaweza kupona kuliko kuchezea maslai ya watu wake wa Mahenge, kamwe hata kubaliana nae.
4-01
Waziri wa Madini Doto Biteko akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili wilayani Ulanga mkoani Morogoro

Mkuu wa Wilaya hiyo Ngollo Malenya alisema uongozi wa wilaya na timu yake wanafurahi kwa uwepo wa wawekezaji  hao, ni imani ya uongozi kuona mchango mkubwa wa kimaendeleo hasa kwenye ulipaji wa kodi ya Halmashauri yetu na utekelezaji wa maendeo kwa ajili ya wananchi. Na Issa Mtuwa – Ulanga

Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI YAJIZATITI KUIMARISHA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA RASILIMALI MADINI

Serikali imedhamiria kuwa na mikakati endelevu ya kusimamia na kudhibiti rasilimali madini ili ilete tija …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *