MADINI NA VIWANDA VYALETA MAGEUZI YA UCHUMI NCHINI

  • Mauzo ya bidhaa nje ya nchi zisizo kuwa za kawaida yameongezeka kwa asilimia 41.9 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwezi  Novemba, mwaka jana.
  • Hayo yamesemwa  Jijini Dodoma  na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari .
  • Dkt. Abbasi amesema kuwa kupitia jitihada mbalimbali zinazochagizwa na Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli zimesaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato, kuongeza mauzo ya bidhaa muhimu kwenda nje na ukuaji wa viwanda nchini  ikiwa ni sehemu muhimu ya  mageuzi ya uchumi nchini.
1-01
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa habari .
  •  “Wote mnafahamu kuwa Serikali imechukua hatua kubwa kuanzisha masoko ya madini na kuzuia uuzaji holela na utoroshaji wa madini. Matokeo yake tumeanza kufaidi. Hadi Novemba, 2019, mauzo ya dhahabu nje ambayo ni asilimia 51.4 ya mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi yaani bidhaa zisizo za kawaida, yaliongezeka kwa asilimia 41.9 kufikia kiasi cha Dola Bilioni 2.1”, alisema Dkt. Abbasi
  • Aidha, aliongeza kuwa  “sera ya kuchagiza ujenzi wa viwanda nayo imezidi kulipa, ambapo  mauzo ya bidhaa za viwandani nje ya nchi  yameongezeka kwa asilimia 28.4 kufikia Dola milioni 996.0 ikichangiwa zaidi na bidhaa za chuma na mabati, vioo, tumbaku, katani na mbolea.
  • Jitihada hizo za Serikali zimeendelea kusaidia kuongeza ajira kwa watanzania, sambamba na kuwa vyanzo vipya vya mapato huku vikitazamiwa kusaida uboreshaji wa huduma za kijamii.Na Immaculate Makilika – MAELEZO
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI KAIRUKI AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.