Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa mamlaka za sheria nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam leo

WIZARA YAZINDUA USHIRIKIANO MAMLAKA KUU SEKTA YA SHERIA

  • Wizara ya katiba na Sheria imezindua ushirikiano wa Mamlaka Kuu za Sheria nchini zitakazokaa pamoja kubainisha uwezo na changamoto zinazoikabili sekta ya sheria nchini na kuzifanyia kazi ili kuongeza ufanisi wa sekta hiyo na hivyo kutoa mchango stahiki kwa taifa.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa mamlaka za sheria nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
  • Ushirikiano huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) na kuhudhuriwa na Jaji Mkuu Mhe. Prof Ibrahim Juma na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome.
  • Akizindua ushirikiano huo Prof Kabudi amewataka wajumbe wa ushirikiano huo kufahamu kuwa wajumbe wote kwa ujumla wao wanajenga nyumba moja na wautumie ushirikiano huo kama chachu na hivyo kuleta tija na ufanisi kwa sekta ya sheria nchini ili iweze kutoa mchango wa kweli kwa Taifa.
Wajumbe wa ushirikiano wa mamlaka
Wajumbe wa ushirikiano wa mamlaka kuu za sheria nchini katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma baada ya uzinduzi wa ushirikiano huo jijini Dar es salaam leo
  • “Sekta hii ni moja, wote hapa mnajenga eneo moja, tumieni ushirikiano huu kama chachu ya kuleta tija na ufanisi kwa sekta hii na muwe huru kushauri na kuzungumza ili kuifanya sekta ya sheria ambayo ni sekta mtambuka kutoa mchango wa kweli kwa taifa hili,” alisema Prof. Kabudi.
  • Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma ameipongeza Wizara kwa  kuanzisha ushirikiano huo hasa ikizingatiwa kuwa sekta ya sheria ndio mama wa sekta zote nchini kwani sekta zote zinatumia sheria kujiendesha.
Waziri wa Katiba na Sheria
Waziri wa Katiba na Sheria mh. rof Palamagamba Kabudi akiwa na Jaji Mkuu wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa mamlaka za sheria nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
  • Amesema Ushirikiano ulioanzishwa utawezesha kuwepo kwa mashauriano baina ya mamlaka za sheria ili pamoja na mambo mengine utawezesha kuwa na msimamo mmoja juu ya masuala mbalimbali na pia utawezesha kutumika kama njia ya haraka ya kutatua changamoto mbalimbali katika sekta na kwa nchi kwa ujumla.
  • “nipongeze kwa kuzindua ushirikiano huu, ni kitu kizuri kitawezesha kufanyika kwa mashauriano kwa pamoja na kutoka na msimamo mmoja kama timu, ushirikiaano huu unaweza kutumika kama njia ya haraka ya kutatua jambo na hivyo kutoa ushauri wa haraka kwa sekta husika kwa taifa na hata kwa uongozi wa nchi,” alisema Prof. Juma.
Waziri wa KAtiba na Sheria
Waziri wa KAtiba na Sheria akizungumza wakati akizundua ushirikiano wa mamlaka za sheria nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
  • Ushirikiano huo unaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Mwenyekiti na wajumbe wake ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma Wizara ya Katiba na Sheria, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria- Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwandishi Mkuu wa Sheria, Mkurugenzi wa Mashtaka, Wakili Mkuu wa Serikali na Kabidhi Wasii Mkuu.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Shria Prof. Sifuni Mchome
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Shria Prof. Sifuni Mchome aliesimama akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa mamlaka kuu za sheria nchini uliozinduliwa na Waziri wa Katiba na Sheria mhe. Prof. Palamagamba Kabudi jijini Dar es Salaam leo
Ad

Unaweza kuangalia pia

DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI KATIKA WILAYA YA KINONDONI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *