RAIS MAGUFULI AIPONGEZA MAHAKAMA NA WADAU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

R2-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020
  • Rais  Dkt. John  Magufuli ameipongeza Mahakama na wadau wake kwa hatua kubwa za kimaendeleo zilizopigwa katika kipindi cha miaka 4 iliyopita na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha Mahakama inaboreshwa zaidi.
  • Rais Magufuli ametoa kauli hiyo tarehe 06 Februari, 2020 katika sherehe za kilele cha Wiki ya Elimu na Siku ya Sheria zilizofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Majaji Wakuu Wastaafu, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, viongozi wa taasisi mbalimbali, viongozi wa Dini na Viongozi wa Siasa.
R3-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020
  • Katika hotuba hiyo, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na mafanikio makubwa ya utekelezaji wa ahadi na maelekezo yake juu ya uboreshaji wa Mahakama yakiwemo kumaliza mrundikano wa mashauri mahakamani na kupunguza mrundikano wa mashauri yenye muda wa zaidi ya miaka 2 kutoka asilimia 12 hadi 5.
  • Mhe. Rais Magufuli amebainisha mafanikio mengine kuwa ni Serikali kuteua Majaji wapya 11 wa Mahakama ya Rufani, Majaji wapya 39 wa Mahakama Kuu na kuajiri Mahakimu wapya 396 ambao wamesaidia kupunguza tatizo la ucheleweshaji wa kesi, na pia amempongeza Waziri wa Katiba na Sheria kwa kuwapa Mahakimu 195 mamlaka ya kusikiliza mashauri ya Mahakama Kuu ambapo Mahakimu 98 walifanya kazi hiyo wamemaliza mashauri 1,132 kwa mwaka jana. Ameahidi kuwaangalia Mahakimu waliofanya kazi hiyo.
R4-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020
  • Aidha, Mhe. Rais Magufuli amepongeza hatua kubwa iliyopigwa na Mahakama katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo licha ya kupunguza tatizo la ucheleweshaji wa kesi na rushwa, pia imesaidia kuongeza maduhuri ya Serikali kutoka shilingi Bilioni 1.6 hadi kufikia shilingi Bilioni 2.5.
  • Maeneo mengine ni kuanzishwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambapo katika maeneo inayofanya kazi idadi ya mashauri imepungua (mfano Mahakama ya Kisutu ambayo mashauri yanayofikishwa mahakamani yamepungua kutoka zaidi ya 1,500 kwa mwaka hadi kufikia 300), kutoa msamaha kwa wafungwa 38,801 hali iliyosaidia kupunguza msongamano magerezani na kuanzishwa kwa Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Ufisadi (Mahakama ya Mafisadi) ambapo tangu ianzishwe mwaka 2016 mashauri 119 yamesajiliwa, 89 yamemalizika, faini iliyolipwa ni shilingi Bilioni 13.6 na fidia shilingi Bilioni 30.6.
R5-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020
  • Kuhusu miundombinu, Mhe. Rais Magufuli amesema kwa miaka 4 Serikali imejenga Mahakama Kuu 2 (Mara na Kigoma), imekarabati Mahakamu Kuu 4 (Dar es Salaam, Shinyanga, Mbeya na Sumbawanga), imejenga Mahakama za Wilaya 15 na Mahakama za Mwanzo 11.
  • Mhe. Rais Magufuli amekiri kuwa pamoja na mafanikio hayo makubwa bado kuna changamoto na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuzishughulikia kadiri uwezo wa kifedha unavyo ruhusu.
R14-01
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akizungumza mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020
  • Ametoa wito kwa Mahakama na wadau wengine yakiwemo Mabaraza ya Ardhi kutoa kipaumbele katika kushughulikia migogoro ya ardhi na dhuluma dhidi ya wanawake hasa wajane ambayo imekithiri hapa nchini. Amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ambao ni wenyeviti wa kamati za mahakama katika maeneo yao kushirikiana vizuri na Mahakama katika kushughulikia kero mbalimbali za wananchi.
R13-01
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Job Ndugai akizungumza mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020
  • Kuhusu kaulimbinu ya mwaka huu isemayo “Uwekezaji na Biashara; Wajibu wa Mahakama na wadau katika kukuza uwekezaji na biashara” Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Mahakama kwa kutambua safari ya Tanzania kujenga uchumi wa viwanda inapoelekea katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
R12-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Spika Job Ndugai ,Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustine Mahiga , Jaji Mkuu wa Zanzibar Omary Othuman Makungu, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020
  • Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa ushirikiano mkubwa ambao Serikali inautoa kwa Mahakama na ameahidi kuwa Mahakama itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi ili kuhakikisha Watanzania wanapata haki yao ipasavyo.
R11-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Spika Job Ndugai ,Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustine Mahiga , Jaji Mkuu wa Zanzibar Omary Othuman Makungu, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyma vya Siasa kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020
  • Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) Dkt. Rugemeleza Nshala amesema TLS iliyotimiza miaka 65 tangu kuanzishwa kwake ina Mawakili 8,667 ambapo takribani asilimia 75 ni vijana. Hivyo kuna hitaji kubwa la kuwajengea uwezo wa kimaadili na uzoefu wa kazi za uwakili na hivyo TLS inahitaji kupata majengo na fedha za kujiendesha, mambo ambayo Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itayaangalia.
R10-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Spika Job Ndugai ,Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustine Mahiga , Jaji Mkuu wa Zanzibar Omary Othuman Makungu, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk katika picha ya pamoja na Mabalozi wanao ziwakilisha nchi mbalimbali hapa nchini kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020
R9-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini Biswalo Mganga kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020.
R7-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai pamoja na Viongozi wengine wakipiga makofi wakati kwaya ya Mahakama ikitumbuiza kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020
R6-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai baada ya hotuba yake kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 6, 2020 (kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma)
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *