Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika hafla kuwaapisha Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani na Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu ,Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 29,2019.

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI

  • Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Islam Seif Salum Mchenga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority – DSFA).
  • Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Mchenga umeanza tarehe 01 Desemba, 2018 na kwamba kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Zanzibar.
  • Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Emmanuel Andrew Sweke kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).
  • Uteuzi wa Dkt. Sweke umeanza tarehe 01 Desemba, 2018 na kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Utafiti wa Uvuvi Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tanzania Livestock Research Institute – TAFIRI) – Kigoma.
  • Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Sebastian W. Chenyambuga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI).
  • Uteuzi wa Prof. Chenyambuga umeanza tarehe 26 Januari, 2019.
  • Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Justinian Rwezaula Ikingura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania – GST).
  • Uteuzi wa Prof. Ikingura umeanza tarehe 18 Januari, 2019.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *