KAMATI YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA IMEIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAWEZESHA VIJANA KUPATA UJUZI STAHIKI

  • Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwawezesha Vijana kupata ujuzi kupitia Programu ya Kukuza Ujuzi inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira.
naibu waziri
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde mwenye kofia.
  • Hayo yamesemwa jana na wajumbe wa kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wakikagua utekelezaji wa mradi wa Kitalu Nyumba ambao umelenga kufikia takribani Vijana 18,800 katika kila Halmashauri nchi nzima ifikapo Juni,2019,pamoja na mradi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Vijana ambayo yanahusisha Vijana 10,000.
MAV-2
Moja ya shamba la mradi
  • “Mradi huu ni muhimu sana katika kuiwezesha nguvu kazi ya Taifa hasa Vijana kuwa na Ujuzi stahiki,Tunaipongeza na Serikali kwa mkakati huu lakini pia tunaitaka ipanue wigo ili kuwafikia Vijana wengi zaidi”Alisema Mh Najma Giga-Makamu Mwenyekiti wa Kamati.

 

naibu waziri
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde mwenye kofia.
  • Aidha wakitoa maelezo ya awali,Manaibu Waziri Ikupa Stellah Alex na Anthony Mavunde waliilezea kamati kwamba huu ni mpango mkakati wa kukuza ujuzi kwa Vijana ili kuwafanya Vijana wa Kitanzania kupata ujuzi stahiki ili kuwawezesha kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.
naibu waziri
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde mwenye kofia.
  • Katika hali ya kuzidiwa na furaha,Mmoja wa wanufaika wa programu ya mafunzo ya Ufundi stadi Bi. Esther Ngallya aliiomba kamati imtafutie nafasi japo ya kumshika Mkono Rais Magufuli kumshukuru kwa namna ambavyo Serikali yake imebadili muelekeo wa maisha yake na kwa sasa amekuwa Fundi mzuri wa umeme na anajiingizia kipato cha uhakika.
MAV-7
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa wa katikati.

 

 

 

 

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

UKARABATI WA KIVUKO CHA MV. PANGANI II WAKAMILIKA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *