SPIKA NDUGAI AZINDUA MTAALA WA KOZI YA SHAHADA YA UCHUMI NA FEDHA YA CHUO CHA IFM

  • Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mnamo tarehe 17 Aprili 2019  katika viwanja vya Bunge ukumbi wa Pius Msekwa Dodoma waliendesha muhadhara  kwa umma unaohusu Mwelekeo wa Upatikasnaji wa chakula- Kukuza Myororo wa Thamani ya Uzalishaji wa Bidhaa zinazotokana na Kilimo kwa chakula Duniani. Baada ya muhadhara huo kulikuwa uzinduzi wa Shahada ya Sayansi ya Uchumi na Fedha katika matukio haya Mgeni Rasmi alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Job Ndugai (MB).
  • Akizumgumza katika muhadhara huo Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Profesa TadeoSsatta, alisema chuo kimeona umuhimu kuendesha mihadhara kwa umma ili kutoa elimu stahiki na kusaidia Serikali ya awamu ya tano katika kukuza sekta ya Viwanda na Uchumi.
SPIKA WA BUNGE
Picha ya Pamoja ya Spika wa Bunge Job Ndugai akiwa na Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga , Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhanga Mpina na Uongozi wa Chuo cha IFM baada ya kumaliza Muhadhara.
  • Pia Prof. Satta, alisema kuongeza shahada hii ya Uchumi na Fedha ikiwa na lengo la kuongeza taifa elimu juu ya Uchumi na Fedha ambayo pia sekta muhimu katika awamu hii ya tano.
  • Alisema kwa sasa chuo kimekua kwa kasi sana na kwa sasa kinaendesha kozi zaidi ya 35 katika fani mbalimbali.
  • Akizumza na hadhara ilioyo hudhuria wakiwemo waheshimiwa Wabunge na wananchi, Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Kilimo, Mifugo na Chakula Mahmoud mgimwa(MB)  alisema IFM kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waliona umuhimu wa chakula nchi hivyo wakaona umuhimu wa  kuwashirikisha wabunge na wananchi wahudhurie mhadara huu muhimu.
  • Mgeni rasmi Spika wa Bunge Job Ndugai (MB) alifurahishwa na IFM kuona fursa yakuwakutanisha pamoja watendaji wa sekta mbalimbali katika masuala ya kuongeza thamani na kuboresha bidhaa zinazotokana na kilimo kubadilishana uzoefu kuhusu namna za kuondokana na changamoto zinazojitokeza katika sekta ya kilimo.
WABUNGE
Baadhi ya Wabunge wakifatilia muhadhara juu ya mwelekeo wa upatikanaji wa Chakula, Kukuza Mnyororo wa thamani ya Uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na Kilimo kwa Chakula Duniani.
  • Pia alisizitiza kwamba Mihadhara kama hii inasaidia kutoa elimu  kuwa ukulima katika kiwango chochote ni sehemu ya biashara. Na shughuli yoyote ya kibiashara inahitaji kuangaliwa katika upana wake ikiwa ni pamoja na kuangalia mnyororo wa thamani, kutoka katika uzalishaji kwenda kwenye usindikaji, soko na mwisho kwa mlaji.
  • Kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais John Pombe Joseph Magufuli imefanya juhudi kubwa inayolenga kufikia hali ya kuwa na usalama wa chakula na viwanda vya uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na kilimo nchini.
  • Mwendesha mhadhara wa mada iliyohusu  mwelekeo wa upatikasnaji wa chakula- kukuza myororo wa thamani ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na kilimo kwa chakula Duniani Profesa Daktari Jan Willem Velthuizen  kutoka Chuo kikuu cha Groningen cha Uholazi, alisema sababu kubwa za upungufu wa chakula unasabishwa na Ongezeko la watu, Mabadiliko ya ladha za vitu, Mabadiliko ya tabia nchi, Uhaba wa maji, Uchumi, Rasilimali na Ukuaji wa miji.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Bw. Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *