WAGONJWA 15 KUPATA MATIBABU YA KUZIBUA MISHIPA YA DAMU YA MOYO

  • Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao wa  Hospitali ya Meditrina ya nchini India wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa  siku tatu ya kuzibua mishipa ya damu  ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa (Chronic Total Occlusion) na hivyo kushindwa kupitisha damu vizuri.
  • Kambi hiyo ni maalum kwa ajili ya  kuwasaidia wagonjwa wenye matatizo hayo ambao bila ya kupata mtaalamu mwenye ujuzi wa hali ya juu wa kuzibua mishipa hiyo wangefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.
  • Matibabu hayo yanafanyika kwa kutumia mtambo wa Cathlab ambapo mgonjwa anatobolewa tundu dogo katika paja ambalo linapitishwa vifaa maalum vya kuzibua mishipa ya damu ya moyo (Stent).
  • Katika kambi hiyo wataalamu wa afya wa JKCI watapata elimu ya jinsi ya kuzibua mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa.
  • Jumla ya wagonjwa 15 ambao mishipa yao ya damu mmoja hadi mitatu imeziba wanatarajiwa kutibiwa  katika kambi hiyo iliyoanza leo tarehe 23 hadi 25/4/2019. Hadi sasa wagonjwa watano wameshatibiwa na hali zao zinaendelea vizuri.

Imetolewa na:

Anna Nkinda

Ad

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Ad

Unaweza kuangalia pia

DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI KATIKA WILAYA YA KINONDONI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *