Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi (kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali zinahusu ofisi ya Katibu Mkuu kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.Ally Possi ikiwa ni sehemu ya makabidhiano ya ofisi mara baada ya kikao na viongozi wa menejimenti aliporipoti Jijini Dodoma.

KATIBU MKUU DKT. ABBASI ASISITIZA MAGEUZI YA KIUTENDAJI KWA MENEJIMENTI

  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi amewataka viongozi wa menejimenti wa Wizara hiyo kufanya mageuzi kwa kuwa sekta za wizara  hiyo zimebeba ushawishi mkubwa kwa nchi  na dunia.
  • Dkt.Abbasi ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma baada kuwasili katika ofisi ya wizara hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba na kufanya mazungumzo na viongozi wa Menejimenti kwa lengo la kupata taarifa fupi ya kisekta na makabidhiano ya ofisi.
4-01
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (kulia) akitoa taarifa fupi kuhusu Idara za Kisekta na Vitengo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.Hassan Abbasi wakati wa kikao cha utambulisho wake kwa viongozi wa menejimenti  Jijini Dodoma, mara baada ya kuapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli.
  • “Wizara hii imebeba sekta muhimu sana katika nchi ambazo ni soft power na smart power mfano sekta ya Sanaa na Michezo ni burudani na sekta hizi zikisimamiwa vizuri taifa hili litazidi kuwa la amani  na furaha pamoja na uchumi utaongezeka,tutaandaa matamasha ya kitaifa ya burudani kama JAMAFEST ambayo yatashirikisha wasanii na wachezaji sisi ni watumishi wa umma lazima tuoneshe wananchi utendaji wetu na ningependa tuache kufanya kazi kwa mazoea,”alisema Dkt.Abbasi.
  •  Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho, Dkt. Abbasi alisema kuwa anatarajia kuona utendaji wa pamoja (team work) na utendaji wa kujituma pasipo kuchoka,pia alisisitiza anategemea kutumia vipaji na ubunifu.
3-01
Katibu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi (kushoto) akisalimiana kwa furaha na wafanyakazi wa wizara alipowasili katika ofisi ya wizara hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma,mara baada ya kuapishwa kwake jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli.
  • Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Ally Possi alipokuwa akifanya makabidhiano alimweleza Dkt. Abbasi changamoto mbalimbali za wizara ikiwemo ya uhaba wa fedha katika uendeshaji wa Uwanja wa Taifa na pamoja na Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kuwa na changamoto katika uendeshaji, umuhimu wa  programu hiyo sababu kuwa ni ya kimataifa na faida zake utakaposimamiwa vyema na kukamilika.
  • “Nakupongeza kwa mapinduzi makubwa unayoyafanya katika Idara ya Habari hakika kazi ni nzuri haswa katika kuisemea Serikali ningeomba kwa upande wa usimamizi wa taaluma ya habari na Vitengo vya Mawasiliano Serikalini huko nako nguvu inahitajika ili kuwa na utendaji wenye usawa katika uwajibikaji wenye tija,’’alisema Dkt.Possi.
2-01
Katibu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi (kushoto) akisitiza kwa viongozi wa menejimenti (hawapo pichani)kuwa amedhamiria kufanya mageuzi ya kiutendaji alipofanya kikao na viongozi hao,baada ya kuwasili katika ofisi ya wizara iliyopo Mji wa Serikali Mtumba,Jijini Dodoma baada ya kuapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli,kulia ni Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo Dkt.Ally Possi.
1-01
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi akipokea zawadi ya ua kutoka kwa mtumishi wa wizara hiyo Bi.Tukupsya Mwamasage alipowasili katika ofisi za wizara Mji wa Serikali Jijini Dodoma, mara baada ya kuapishwa jana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli.
  • Aidha, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw.Marceline Patrick alimpongeza Katibu Mkuu huyo na kumweleza kuwa watumishi wote wamefurahia uteuzi wake na wana imani nae katika kusimamia mabadiliko ya sekta za wizara na wapo tayari kumpa ushirikiano ili kufanikisha hilo.
  • Halikadhalika  mmoja wa wafanyakazi wa wizara hiyo kutoka Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Bibi Hadija Kisubi alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt.John Pombe Magufuli kwa kumteua Dkt.Abbasi kuwa Katibu Mkuu katika wizara hiyo sababu ni mchapakazi na anaamini kuwa atafanya mabadiliko makubwa katika wizara katika maeneo yote yenye changamoto.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MWAKYEMBE AWATAKA WATANZANIA KUJITOKEZA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA MICHEZO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa watanzania wanaoishi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *