SERIKALI YAKUSANYA KODI YA SH.BILLION 5.5 ZA TAULO ZA KIKE

  • Sserikali imesema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2017/18 ilikusanya kodi ya ongezeko la thamani(VAT) ya kiasi cha Sh. Bilioni 5.5 kwenye bidhaa ya taulo za kike ‘Sanitary Pads’ zilizoingizwa nchini kabla ya kodi hiyo kuondolewa Juni mwaka jana.
  • Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum(Chadema), Upendo Peneza.
  • Katika swali lake, Peneza alitaka kujua katika mwaka wa fedha 2016/17 na 2018/19 serikali ilikusanya kiasi cha kodi ya asilimia 18 kwa taulo za kike ’Sanitary pads’ zote zilizotengenezwa hapa nchini na zilizoingia kabla ya kodi ya VAT kuondolewa.
  • Akijibu swali hilo, Dk.Kijaji alisema katika mwaka wa fedha 2016/17 serikali ilikusanya VAT ya kiasi cha Sh. Bilioni 3.01 na Sh.Bilioni 2.54 kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwenye bidhaa ya taulo za kike zilizoingizwa nchini.
  • Alisema pia zile zilizozalishwa hapa nchini kabla ya kodi hiyo kuondolewa Juni, 2018.
  • Katika swali la nyongeza, Mbunge huyo alihoji japokuwa kodi zimeondolewa kwenye taulo ya kike bado bei ipo juu je ina mpango gani kusimamia suala hilo ili bei zishuke.
  • Dk. Kijaji alisema serikali ipo kwenye soko huru kwa bidhaa zote na kwamba haijashindwa kusimamia na ndio maana baada ya kuondoa kodi wameendelea kupokea maoni.
  • Kadhalika, alisema utafiti unafanyika na wameenda nchi za Afrika Kusini, Botswana na Kenya ambazo walifanya hivyo lakini waligundua hatua hiyo haiwezi kuleta matokeo chanya.
  • “Hivyo tunatakiwa kuhakikisha wanapewa taulo hizo bila kuhusishwa na kodi, tutafanya utafiti na tukijiridhisha kama watoto wetu wanaweza kupewa hivyo alivyotaka Mbunge tutaleta ombi maalum bungeni,”alisema.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SHIRIKA LA IFC LATAKIWA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KATIKA UCHAMBUZI WA MAZINGIRA YA SEKTA BINAFSI

Serikali ya Tanzania imeiomba Benki ya Dunia kupitia Shirika lake la Fedha (IFC), kufanya kazi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *