URAFIKI WETU TANZANIA NA CHINA UNA FAIDA NA MAFANIKIO MAKUBWA – PROF. NDALICHAKO

 • Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, zimeadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia ulioasisiwa na Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mao Ze Dong, Rais wa kwanza wa  China.
CHINA
Balozi wa China Nchini Tanzania Wang Ke, akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019
 • Akiongea katika maadhimisho hayo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, amesema kuwa uhusiano huo umejenga urafiki mkubwa kwa Tanzania na China katika Nyanja zote za maendeleo.
NDALICHAKO-
Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekenolojia, Prof. Joyce Ndalichako Akizungmza katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China,iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019
 • “Napenda kuanza na Nukuu ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere ambaye alisema kuwa “sisi tunataka kuwa rafiki wa kila mtu na hatuwezi kuwa na rafiki ambaye anatuchagulia adui yetu”, China ilionyesha dhamira ya kuwa rafiki wa Tanzania, rafiki ambaye tulizuiwa kuwa rafiki yetu kipindi cha ukoloni, maneno haya ya Baba wa Taifa yalionyesha namna gani alivyokuwa anathamini urafiki wa Tanzania na China, kwa hiyo China ni rafiki yetu mkubwa”. Amesema Prof. Ndalichako.
NDALICHAKO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekenolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki, Dkt. Damas Ndumbaro na Katibu Mkuu CCM, Dkt.Bashiru Ally katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wakidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019
 • Prof. Ndalichako ameeleza kuwa miaka 55 ya uhusiano huo umechochea kuwa na urafiki mkubwa ambao umeleta faida kwa kila nchi kwa sababu ya kujenga historia kubwa, kuthaminiana, kuheshimiana, kwa hiyo huo ni urafiki ambao kila mtu anamuheshimu mwenzie.
NDALICHAKO
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda na mkewe Tunu Pinda, wakifuatilia hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpyaya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019
 • Prof.Ndalichako amesema kuwa katika maadhimisho ya miaka 55 kumekuwa na mafanikio makubwa katika Nyanja ya kiuchumi kwa kuwepo na miradi mbalimbali inayotokana na uhusiano China na Tanzania, miradi ambayo imetekelezwa ni Reli ya TAZARA, Kiwanda cha Urafiki, Kiwanda cha UFI, Kiwanda cha dawa keko, Kiwanda cha sukari Mahonda Zanzibar na Shamba la mpunga Mbarali.
NDALICHAKO
Wasanii kutoka China wakitoa burudani katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019
 • Miradi mingine iliyotekelezwa kwenye urafiki huo ni Uwanja cha mpira wa Taifa, Uwanja wa mpira Amani Zanzibar, Bwawa la maji Chalinze, Kituo cha Mikutano Julius Nyerere, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Maktaba ya Chuo Kikuu Dar es Salaam ambayo ni maktaba kubwa kuliko zote ukanda wa Afrika pamoja na jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 • Prof. Ndalichako amesema kuwa China imekuwa ikiifadhili Tanzania nafasi 100 za wanafunzi kusoma China katika fani mbalimbali zikiwemo za uhandisi na udaktari

 

NDALICHAKO
Wasanii kutoka China wakitoa burudani katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019.
 • “Kila mwaka China imekuwa ikitoa nafasi 100 kwa wanafunzi wetu kusoma nchini China, lakini pia katika maeneo muhimu kama udaktari kuna nafasi 20 za madaktari bingwa kwenye fani ya upandikizaji uboho na nafasi 30 kwa madaktari kwenda kusoma mafunzo mafupi, hakika huu ni urafiki mzuri na umekuwa na mafanikio makubwa”, amesema Prof.Ndalichako.
 • Kwa upande wa Miradi ya uwekezaji Prof.Ndalichako amesema kuwa tokea mwaka 1990 hadi Desemba mwaka jana tayari China ina miradi 723 ambayo imefanywa na wawekezaji kutoka China ambayo imetengeneza ajira 87,126, pia kwenye utalii Tanzania na China zimekuwa zikishirikiana kwa muda mrefu sasa.
NDALICHAKO
Kikundi cha ngoma za asili kutoka Mwananyamala Jijini Dar es Salaam, kikitoa Burudani katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019. (Picha na: Paschal Dotto-MAELEZO).
 • “Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano mkubwa pia katika sekta ya utalii na sekta ya utamaduni, ikiwemo kwa Chuo chetu cha Dar es Salaam na Dodoma kuwa na taasisi za kufundisha utamaduni wa China, lakini pia tumeanza kufundisha lugha ya kichina na mpaka sasa shule 15 zinafundisha lugha hiyo, kwenye utalii uzinduzi wa safari ya ndege yetu ya Dreamliner 787 itaanza safari zake moja kwa moja mpaka China na kuleta watalii wengi kutoka china kuja kutalii nchini”.
 • Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke alisema kuwa uhusiano huo ulioasisiwa na  Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania na Mao Ze Dong Rais wa kwanza wa  China, umeleta urafiki mkubwa kwa watu wa Tanzania na China.
 • “Hatuna budi kuulinda urafiki huu kwani ni urafiki wa faida, tumekuwa tukishirikiana katika miradi mbalimabli ikiwemo ujenzi wa reli ya TAZARA na miradi mingine ya maendeleo ambayo inaleta faida na manufaa kwa watu wetu”, alisema Wang Ke.
 • Urafiki wa Tanzania na China ulianza mwaka 1964 mara baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana na kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MWANAFUNZI WA MALANGALI AINGIA KUMI BORA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

#SisiTumeona SISI WATANZANIA TUNAWEZA Hivi sasa watoto wetu wanapata elimu bure bila malipo! ——————————— Matokeo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *