Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano (wanne kutoka kulia) Mstahiki Meya wa Jiji Mh. Isaya Mwita, akifuatiwa na Prof. Charles Majinge, Prof. Lawrence Museru (wanne kutoka kushoto) akifuatiwa na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.

KONGAMANO LA KWANZA LA KISAYANSI KUHUSU KUTAFSIRI TAFITI KWA VITENDO LA FUNGULIWA DAR.

  • Wataalam wa afya nchini wametakiwa kujikita zaidi katika kufanya utafiti na uvumbuzi ili kuleta matokeo chanya katika utoaji wa huduma za afya.
  • Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Charles Majinge wakati akifungua kongamano la kwanza la kisayansi kuhusu kutafsiri tafiti kwa vitendo katika kutoa huduma za tiba lililofanyika Hospitali ya Mloganzila.
  • Prof. Majinge amesema utafiti na uvumbuzi ndio mwelekeo wa dunia nzima katika kuhakikisha huduma za afya zinazotolewa zina kuwa na tija na rasilimali zinatumika vizuri.
M 1-01
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Charles Majinge akifungua kongamano la kwanza la kisayansi kuhusu kutafsiri tafiti kwa vitendo katika kutoa huduma za tiba lililofanyika Hospitali ya Mloganzila na kuhudhuriwa na wataalam mbalimbali wa afya.
  • Amewataka wataalam wa afya nchini kuendelea kufanya utafiti wa kuvumbua namna ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali badala ya kusubiri wataalam kutoka nje kuja kutupatia ufumbuzi.
  • Kwa mujibu wa Prof. Majinge, tafiti zimeonyesha kuwa kutengeneza miongozo na vipaumbele kwenye sekta ya afya ambavyo vimetokana na tafiti zilizofanyika kwenye eneo husika inaokoa fedha nyingi, hiyo inatokana na ukweli kwamba si kila muongozo huleta matokeo chanya katika afya na hivyo kuwa na uhakika wa miongozo inayotolewa ambayo ina uwezo wa kuleta matokeo chanya ni muhimu.
  • “Ili huduma bora zitolewe, pamoja na uhaba wa rasilimali watu na rasilimali fedha ni muhimu kutafuta njia mbadala zenye uwezo wa kupata matokea mazuri pasipo kutumia rasilimali hizo kwa wingi ikiwa na maana ya kugundua njia bora zaidi za utoaji huduma bila kuongeza gharama” amesema Prof. Majinge.
MH
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- Prof. Lawrence Museru akizungumza katika kongamano lililofanyika mapema leo Hospitali ya Mloganzila.
  • Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema Uongozi utaendelea kuweka miundombinu imara kwa wataalam wake ili kuwezesha kufanya tafiti mbalimbali za afya hatua itakayoendelea kuboresha utoaji wa huduma na jamii kujua nini ambacho hospitali inafanya.
M 3-01
Mkuu wa Kitengo cha Elimu na Utafiti Muhimbili Dkt. Faraja Chiwanga akifafanua kuhusu tatifi zinazofanywa na wataalam wa afya.
  • “Tafiti za afya zinasaidia sana kuboresha huduma za tiba tunazozitoa lakini kwa bahati mbaya suala hili halipewi uzito unaotakiwa hivyo tunapaswa kubadilika ili tuendane na wakati na kutoa fursa kwa watu kujua nini kinafanyika MNH’’ amesema Prof. Museru.
MH
Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa katika kongamano la kisayansi hii leo.
  • Amewataka wataalam kubadilika na kuacha hulka ya kusema mimi najua na kukaa miaka kadhaa bila ya hicho anachokijua kukiweka kwenye maandishi kwa faida ya watu wengine kujifunza.
MH
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Mwita akitoa neno kwa washiriki wa kongamano lililohusu kutafsiri tafiti kwa vitendo katika kutoa huduma za tiba.
  • Katika kongamano hilo matokeo ya tafiti mbalimbali yamewasilishwa na wataalam wa afya kutoka MNH Upanga na Mloganzila, ambapo moja ya tafiti hizo ni kuhusu visababishi hatarishi kwa wauguzi wa fya ya akili katika wodi ya magonjwa ya akili Hospitali ya Taifa Muhimbili.
  • Kongamano kuhusu utafiti katika huduma za afya litakua likifanyika mara mbili kwa mwaka katika Hospitali ya Muhimbili.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *