WADAU WA KUANDAA MPANGO KAZI WA PILI WA KITAIFA WA HAKI ZA BINADAMU 2019-2023 WAKUTANA

  • Wadau wa kuandaa Mpango Kazi wa Pili wa Kitaifa wa Haki za Binadamu 2019-2023 wanakutana kama kamati kupitia maoni ya mtaalamu mshauri kwa ajili ya kuandaa mpango huo.
  • Kikao hicho kinafanyika mjini Singida kimefunguliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome ambaye amewataka wadau hao wahakikishe wanatoka na vitu vichache  vinavyotekelezeka na ambavyo vitatoa picha nzuri ya utekelezaji kwa nchi.
KB 2-01
Mjumbe wa kikao cha kuandaa Mpango kazi wa pili wa kitaifa wa haki za binadamu kutoka Zanzibar bi Fatma Hemed akiwasilisha kitu mbele ya Katibu Mkuu Prof.Mchome wakati was ufunguzi wa kikao hicho.
  • “Tusiwe na mambo mengi ambayo yatakuja kuleta shida katika utekelezaji, mkumbuke kuwa suala la haki za binadamu lina vitu vingi sana, tujipange kwa yale ambayo yatatuwezesha kutoka na taarifa bora ya utekelezaji wetu mbele ya dunia,” alisema Prof. Mchome
  • Amesema suala la kukuza na kulinda haki za binadamu ni suala la msingi ambalo Serikali inatekeleza ikizingatiwa makubaliano ya kimataifa ambayo kama nchi iliyaridhia.
KB 1-01
Wajumbe wa kikao cha kuandaa Mpango kazi wa pili wa kitaifa wa haki za binadamu wakimsikiliza Katibu Mkuu Prof.Mchome wakati akifungua kikao hicho
  • Mpango Kazi wa Haki za Binadamu utawezesha vipaumbele vya nchi kuhusu masuala ya haki za binadamu kujulikana, pamoja na kubainisha namna ya kutekeleza katika kukuza, kulinda na kuendeleza haki za binadamu nchini.
  • Zoezi la uandaaaji wa Mpango Kazi wa Pili wa Kitaifa wa Haki za Binadamu lilianza Oktoba 2018 ambapo Wizara ya Katiba na Sheria, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa Kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa kupitia Wataalamu Waelekezi walikusanya maoni kutoka kwa makundi mbalimbali wakiwemo Wadau kutoka Serikali za Mitaa; Wadau Kutoka Taasisi za Kidini; Asasi za Kiraia, Vyombo vya Habari; na Wananchi ili kupata vipaumbele vya kuingiza katika Mpango Kazi huu.
  • Mpango Kazi wa Kwanza wa Kitaifa wa Haki za Binadamu wa 2013-2017 ulimalizika 2018.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *