Daktari wa macho wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Geofrey Josephat akitumia kifaa maalum kumfanyia uchunguzi mtoto sehemu ya nyuma ya jicho ili kubaini kama ana tatizo. Hospitali ya Mloganzila imefanya zoezi la uchunguzi wa macho bure kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya saratani ya jicho kwa watoto (Retinoblastoma).

ZAIDI YA WATOTO 100 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MACHO MLOGANZILA

EYE
Mtaalam wa miwani Nestory Massawe akimpima uwezo wa kuona mbali mtoto Shamsa Mbegu.
  • Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imefanya zoezi la uchunguzi wa macho bure kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya saratani ya jicho kwa watoto (Retinoblastoma).
  • Katika zoezi hilo ambalo limefanyika Mei 16 hadi Mei 17, 2019 zaidi ya watoto 100 wamehudumiwa ambapo baadhi yao wamekutwa na matatizo ya uoni hafifu, mzio na kovu kwenye macho.
EYE
Daktari Bingwa wa macho Suzan Mosenene (kulia) akimfanyia uchunguzi wa macho mtoto, huduma ya uchunguzi wa macho bure kwa watoto imefanyika Mei 16 hadi Mei 17, 2019.
  • Daktari Bingwa wa macho kutoka Muhimbili Judith Mwende amesema ugonjwa wa saratani ya jicho kwa watoto ni hatari na husababisha upofu na kifo endapo usipotibiwa mapema na wakati mwingine hulazimu kuliondoa jicho ili kuokoa  maisha ya mtoto.
  • Akifafanua Dkt. Mwende amesema takwimu za miaka mitatu za kutibu na kufuatilia ugonjwa wa saratani ya jicho  kwa watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) takribani asilimia 60-70 ya watoto hao huwa wako kwenye hatua mbaya za ugonjwa.

EYE

  • Hali hiyo husababisha asilimia 50-60 kupoteza maisha kwa sababu ya kuchelewa kufika kupata huduma inayostahili na kwa wakati.
  • Ametaja  sababu za kucheleweshwa hospitalini ni familia kutokufahamu dalili za  ugonjwa  na hatari zake, wahudumu wa afya ya msingi kuchelewesha rufaa kwa kutofahamu dalili za ugonjwa, familia kukosa nauli kufuata matibabu pindi wakipewa rufaa , familia kutafuta matibabu mbadala mpaka wakiona hatua za mwisho za ugonjwa na kukataa mapendekezo ya wataalam hasa kuliondoa jicho pale inapohitajika ili kunusuru maisha ya mtoto
  • Dalili za mwanzoni za saratani ya jicho kwa watoto ni weupe kwenye mboni ya jicho ambao unaonekana kirahisi kwenye giza au mtoto akipigwa picha na flush, kengeza, jicho kuvilia damu kuwa jekundu, kubadilika rangi au kuuma.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *