RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA RAIS WA DRC MHE. THISEKEDI ALIYEHITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI NCHINI LEO

  • Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antoine Tshisekedi amemaliza Ziara ya Kitaifa ya siku 2 aliyoifanya hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
  • Mhe. Tshisekedi ameagwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuelekea nchini Burundi.
RA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wakatia aikondoka Ikulu kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili leo Juni 14, 2019
  • Mapema leo asubuhi Mhe. Rais Tshisekedi ametembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge Railway) katika eneo la Vingunguti Jijini Dar es Salaam na baadaye akatembelea Bandari ya Dar es Salaam ambayo hutumika kupitisha mizigo ya DRC.
RA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo anayeagana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa afrika Mashariki Mhe. Faraji Kasidi Mnyepe baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019
  • Akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais Tshisekedi amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli na baadaye viongozi hao wamezungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari.
RA 9-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo anayeagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili leo Juni 14, 2019
  • Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Tshisekedi kwa kufanya Ziara ya Kitaifa hapa nchini na kwa dhamira yake ya kukuza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya DRC na Tanzania hususani katika uchumi.
  • Mhe. Rais Magufuli amesema kiwango cha biashara kinachofanywa kati ya Tanzania na DRC ni kidogo ikilinganishwa na ukubwa wa uhusiano na fursa zilizopo kati ya nchi hizo, ambapo katika mwaka uliopita biashara kati ya Tanzania na DRC ilikuwa na thamani ya shilingi Bilioni 305.375, wafanyabiashara wa DRC walikuwa wamewekeza nchini Tanzania miradi 8 yenye thamani ya shilingi Bilioni 13.144 na kukiwa na Watanzania wachache ambao wameweka nchini DRC.

RA

  • Amefafanua kuwa japo kuwa sekta ya usafirishaji inaridhisha kidogo kwa DRC kuongeza mizigo inayopita Bandari ya Dar es Salaam kutoka tani Milioni 1.176 ya mwaka 2017 hadi kufikia tani Milioni 1.78 ya mwaka 2018, kuna haja ya kuchukua hatua madhubuti zaidi za kukuza biashara na uwekezaji ikiwemo kuondoa vikwazo, kutumia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo madini, uvuvi, kilimo, ujenzi wa viwanda na kulitumia ipasavyo soko la nchi hizo lenye jumla ya watu Milioni 140.
  • Kwa upande wa Tanzania, Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kujenga reli ya kati (SGR), kupanua Bandari ya Dar es Salaam, kuanzisha huduma za pamoja za bandari kwa saa 24 (siku zote 7 za wiki) na kuimarisha miundombinu ya barabara katika njia 8 za kuingia na kutoka DRC, Tanzania imeongeza muda wa kusubiri bandarini kutoka siku 24 hadi 30 kwa mizigo ya DRC, imeondoa katazo la ufunguaji makontena na kufuta tozo ya kusindikiza mizigo hadi mpakani mwa Tanzania na DRC.

RA 1-01

  • Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema Tanzania itaikarabati meli ya MV. Liemba inayotoa huduma kati ya Tanzania (Kigoma) na DRC, itajenga meli mpya mbili ambapo moja itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na mizigo tani 400 na ya pili itakuwa meli ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 2,000 na ameafiki mapendekezo ya Mhe. Rais Tshisekedi ya reli ya kati ya Tanzania kujengwa kutoka Isaka – Rusumo – Kigali hadi Mashariki ya Kongo ili kufikisha mizigo moja kwa moja nchini DRC.
  • Mhe. Rais Magufuli amewataka Mawaziri na Wataalamu wa Tanzania na wenzao wa DRC (watakaoteuliwa) ndani ya mwaka huu, kuitisha kikao cha Kamati ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission – JPC) ambacho hakijawahi kufanyika tangu mwaka 2002 ili kujadili na kurejesha maeneo muhimu ya ushirikiano ikiwemo ushirikiano katika usafiri wa anga kati ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na Shirika la Ndege la Congo (Congo Airways).
RAIS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana kwa furaha na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia 54 ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili leo Juni 14, 2019
  • Mhe. Rais Magufuli amemtakia heri Mhe. Rais Tshisekedi katika uongozi wake na amemshauri kusimama kidete kutatua matatizo ya wananchi wa DRC huku akisisitiza kuwa kwa utajiri wa DRC, uchumi wa nchi hiyo haupaswi kukua kwa kiwango kidogo cha asilimia 4.
  • Kwa upande wake, Mhe. Rais Tshisekedi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumwalika kufanya Ziara ya Kitaifa hapa nchini na amebainisha kuwa lengo la ziara yake ni kuimarisha na kukuza zaidi udugu, urafiki na uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na DRC.
RA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana kwa furaha na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia 54 ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili leo Juni 14, 2019
  • Mhe. Tshisekedi amesema katika mazungumzo yake na Mhe. Rais Magufuli wamekubaliana kuwa bila amani jitihada za maendeleo katika eneo lote la maziwa makuu hazitafanikiwa, hivyo wana kila sababu ya kuhakikisha kunakuwa na amani ya kudumu pamoja na kutumia vizuri fursa mbalimbali za kukuza uchumi ukiwemo ukanda wa ziwa Tanganyika wenye urefu wa kilometa 554.
RAIS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019
  • Amesema ana matumaini kuwa JPC itakayofanyika itatatua changamoto zote za kukuza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na DRC na ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Mhe. Rais Magufuli.
RA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda wakati wakisumbiri ili kumuaga mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019
  • Pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa ahadi yake ya kuunga mkono ombi la DRC kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Rais Tshisekedi ameahidi kuhudhuria Mkutano wa 39 Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu hapa Tanzania na amebainisha kuwa anaamini kuwa SADC ni jumuiya yenye fursa na manufaa makubwa ya kiuchumi.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA DAR ES SALAAM ZOO, AVUTIWA NA WANYAMA WENGI WANAOFUGWA HUMO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *