BUNGE LAWAALIKA WADAU KUTOA MAONI JUU YA MAAZIMIO YALIYOWASILISHWA NA SERIKALI

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzana linawaalika Wadau kutoa maoni kuhusu Maazimio yaliyowasilishwa na Serikali kwa Mheshimiwa Spika kabla Maazimio hayajaridhiwa na Bunge katika Mkutano wa Kumi na Sita (16) unaoendelea Jijini Dodoma. Maazimio hayo yameelekezwa kwenye Kamati zifuatazo;-
Mosi, Tarehe 05 Septemba, 2019 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji itapokea maoni ya wadau kuhusu Azimio la Bunge kuridhia Itifaki ya Maedeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika kuhusu kulinda Hakimili na Wagunduzi wa Aina mpya za Mbegu za Mimea. (The Protocol for Protection of New Varieties of Plant [Plant Breeder’s Rights] in the Southern African Development Community-SADC).
Kikao cha kupokea maoni ya Wadau kuhusu Azimio hili kimepangwa kufanyika saa 7:00 Mchana katika ukumbi Na. 43 ulioko Jengo la Utawala Annex-Ofisi Kuu ya Bunge, Dodoma.
Pili, Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira itapokea maoni ya Wadau kuhusu Maazimio matatu kama ifuatavyo;
Tarehe 05 Septemba, 2019 maoni ya Wadau kuhusu, Azimio la Kuridhia Itifaki ya Marrakesh inayowezesha Upatikanaji wa Kazi zilizochapishwa kwa Watu Wasioona, Wenye Uoni Hafifu au Ulemavu unaomfanya Mtu kushindwa kusoma ya Mwaka 2013 (The Marrekesh Treaty to Facilitate Access to Published Works for Persons who are Blind, Visually Impaired or Otherwise Print Disabled (MVT) 2013).
Tarehe 06 Septemba, 2019 maoni ya Wadau kuhusu Azimio la Kuridhia Mkataba wa Minamata kuhusu Zebaki (Minamata Convention on Mercury); na
Tarehe 06 Septemba, 2019 maoni ya Wadau kuhusu, Azimio la Kuridhia Itifaki ya pamoja ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusu Uwajibikaji Kisheria na Faida kwa Madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya Bioteknolojia ya Kisasa katika kutekeleza Itifaki ya Cartagena (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety).
Vikao vya Kamati hii kupokea maoni ya Wadau kuhusu maazimio haya vimepangwa kufanyika saa 7:00 Mchana katika ukumbi Na. 49 ulikoko Jengo la Utawala Annex-Ofisi Kuu ya Bunge, Dodoma.
Tatu, Tarehe 05 Septemba, 2019 Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii itapokea maoni ya Wadau kuhusu Maazimio yafuatayo;
Azimio la kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Selous kuwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.
Azimio la kuridhia mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Kigosi kuwa Hifadhi ya Taifa ya Kigosi.
Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji wa Hadhi sehemu ya eneo la Pori la Akiba la ugalla kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto ugalla
Vikao vya Kamati hii kupokea maoni ya Wadau kuhusu maazimio haya vimepangwa kufanyika kuanzia saa 7:00 Mchana katika ukumbi Na. 41 ulikoko Jengo la Utawala Annex-Ofisi Kuu ya Bunge, Dodoma.
Kwa kuzingatia umuhimu wa Maazimio haya, Kamati zinawaalika Wadau wote wenye maoni kuhusu Maazimio haya kufika na kuwasilisha maoni yao kabla hayajapelekwa katika hatua nyingine. Maoni ya Wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya posta au Baruapepe kwa anuani ifuatayo:-
Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA.
Baruapepe ca*@bu***.tz
Imetolewa na: – Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA.
04 Septemba, 2019
Ad

Unaweza kuangalia pia

MATUKIO YA WAZIRI MKUU BUNGENI MJINI DODOMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *