WAZIRI KALEMANI AAGIZA BEI YA GESI ASILIA IPITIWE UPYA

 

  • Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameziagiza Mamlaka zote zinazohusika na upangaji wa bei ya gesi asilia, kufanya mapitio upya ili kuja na bei itakayozinufaisha pande zote yaani serikali na wawekezaji.
UU A-01
Matukio mbalimbali wakati Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Ujumbe wake, wakikagua kiwanda cha kutengeneza vigae cha Goodwill, kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani, Septemba 24, 2019
  • Alitoa maelekezo hayo kwa nyakati tofauti, Septemba 24 mwaka huu, alipofanya ziara katika kiwanda cha kutengeneza vigae cha Goodwill na kiwanda cha kufua vyuma cha Lodhia, vilivyopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani.
  • Dkt Kalemani alitoa muda wa mwezi mmoja kuanzia siku hiyo kwa uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wataalamu wa Wizara, kufanya mapitio ya bei za gesi viwandani ili ziwawezeshe wawekezaji kuzalisha kwa tija.
UU C-01
Matukio mbalimbali wakati Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Ujumbe wake, wakikagua kiwanda cha kutengeneza vigae cha Goodwill, kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani, Septemba 24, 2019
  • Alisema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wawekezaji mbalimbali wenye viwanda, wakiwemo Goodwill na Lodhia, kuwa gharama ya gesi asilia iko juu hivyo wanaomba serikali iangalie uwezekano wa kuipunguza ili wazalishe kwa tija zaidi.
  • “Lengo la serikali ni kujenga mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi kuwekeza nchini hivyo naagiza muanze mara moja kufanya mapitio ya bei husika. Mje na bei linganifu ili kila upande unufaike.”
UU D-01
Matukio mbalimbali wakati Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Ujumbe wake, wakikagua kiwanda cha kutengeneza vigae cha Goodwill, kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani, Septemba 24, 2019
  • Katika kufanya mapito husika, Waziri aliwataka wataalam hao, pamoja na mambo mengine, kuangalia pia uzoefu wa nchi nyingine zenye gesi asilia.
  • Hata hivyo, Waziri alilazimika kufafanua sababu zinazopelekea bei ya gesi kutofautiana katika maeneo mbalimbali, ambapo alieleza kuwa mojawapo ni kutokana na gharama ya kazi inayofanyika katika kuitafuta, kuichimba na hatimaye kuileta juu ya ardhi. Alisema teknolojia husika ina gharama kubwa.
UU E-01
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na uongozi wa kiwanda cha vigae cha Goodwill, kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani, Septemba 24, 2019
  • Pia, alieleza sababu nyingine kuwa ni gharama ya usafirishaji wa gesi kutoka kwenye kisima kwenda kwenye Mtambo maalum wa kuchenjulia pamoja na gharama ya kufanya zoezi hilo la uchenjuaji.
  • “Sasa, kadri unavyokuwa mbali kutoka kwenye eneo la kuchakata gesi, ndivyo gharama inavyoongezeka. Bei ya gesi kwa yule aliye karibu na eneo la uchenjuaji haiwezi kulingana na aliye mbali.”
  • Bei ya sasa ya gesi asilia inaanzia Dola 4.7 hadi 7.72 kwa uniti moja. Na Veronica Simba – Pwani
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *