MADAKTARI BINGWA WA WATOTO WA TAASISI YA MOYO (JKCI) NA PROF. PAN XIANG BIN WAFANYA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA KUPITIA MSHIPA WA DAMU WA KWENYE PAJA

 

1-01
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani na wenzake kutoka Jamhuri ya watu wa China wakimpima mtoto kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiogram) kabla ya kumfanyia upasuaji mdogo wa kuziba tundu la moyo  kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja kwa kutumia mashine ya (ECHO machine)  bila ya  kutumia mionzi (Transthoracic Echocardiography – TTE). Mara nyingi upasuaji huo hufanyika kwa njia ya mionzi kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory).
2-01
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Jamhuri ya watu wa China Prof. PAN Xiang Bin akimfanyia mtoto mwenye umri wa miaka minne ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) upasuaji mdogo wa kuziba tundu la moyo bila kufungua kifua kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja kwa kutumia mashine ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO machine) bila ya kutumia mionzi (Transthoracic Echocardiography – TTE). Mara nyingi upasuaji huo hufanyika kwa njia ya mionzi kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory). Picha na JKCI

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *