TANZANIA YAONGEZA HIFADHI SITA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU

  • Na Pamela Mollel,Ngorongoro
  • Tanzania imeongeza hifadhi sita (6) kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka hifadhi za Taifa 16 hadi 22 hivi sasa.
  • Hayo yalisemwa na Kamishna Mkuu wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi kama moja ya mafanikio kwenye kongamano la watafiti wa masuala ya uhifadhi, kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya hifadhi ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro.
  • Alisema ongezeko la hifadhi hizo ni kuishi ndoto ya uhifadhi wa baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, wakati tunapata uhuru kulikuwa na hifadhi tatu ambazo ni Serengeti inayotimiza miaka 60, Manyara na hifadhi ya Arusha.
  • “Mbali na ongezeko hili la hifadhi lakini pia tunafika kilele hiki cha maadhimisho Serengeti ikiwa hifadhi bora barani Africa” alisema Kamishna Kijazi
  • Kwa upande wa Naibu kamishna wa hifadhi ya mamlaka ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Asangye Bangu alieleza mafanikio waluyo yapata kwa kipindi cha miaka hii 60 ikiwa ni pamoja na ongezeko la watalii wanaotembelea eneo hilo laki saba (700,000) ambao ni karibu ya nusu ya watalii wote wanaokuja nchini.
  • “Tumeweza kutoa gawiwo serikalini la Billion 43, tumeweza kuwasaidia kielimu watu wapatao 6 elfu kwa ngazi mbalimbali licha ya changamoto kadhaa ikiwemo ongezeko la watu katika eneo la hifadhi ambao wamefikia laki moja (100000) na mifugo iliyofikia laki nane (800000) alifafanua zaidi Prof. Abuid Kaswamila M/kiti ya bodi ya wakurugenzi (NCAA)
  • Awali akifungua kongamano hilo mkuu wa mkoa wa Mara Mh. Adam Malima aliwasihi washiriki ambao walitoka makundi ya wanaotoa huduma za utalii, taasisi za mafunzo, zinazofanya tafiti, wanafunzi na wafugaji kutumia nafasi hiyo kushiriki na si wasikilizaji ili kutoa suluhisho la pamoja la changamoto zinazokabili eneo hilo na hifadhi za Taifa kwa ujumla wake.
  • Hata hivyo kongamano hilo lilojadili namna ya kukabiliana na magonjwa yanayotokana na mwingiliano wa wanyama, Ikolojia ya Serengeti Mara, Utalii na ukarimu, Uhusika wa jamii kwenye uhifadhi na utalii wa malikale, litafuatiwa na kilele cha miaka 60 ya hifadhi hizo December 23 eneo la Fort Ikoma nje kidogo ya hifadhi ya Serengeti.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ZANZIBAR NA ANGOLA KUSHIRIKIANA KWENYE SEKTA YA UTALII

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameupongeza uwamuzi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.