Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kuwaapisha katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020

NENDENI MKATANGULIZE UZALENDO KWANZA – RAIS MAGUFULI

  • Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi walioapishwa kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za uongozi pamoja na kuwa na   hofu ya Mungu bila kusahau kutanguliza Uzalendo katika kuhakikisha Tanzania inafikia malengo iliyojiwekea.
  • Rais Magufuli Ameyasema hayo leo tarehe 3 Februari 2020 katika hafla ya Uapisho wa Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.
  • “niwapongeze sana kwa majukumu yenu mapya ambayo nina amini mtakwenda kuyafanyia kazi kwa Uzalendo wa Kweli na bila Kusahau Kumtanguliza Mungu  na kufanya kazi kwa kufuata sheria  katika utendaji kazi wenu huko mnapoenda”  amesema Rais Magufuli
  • Sambamba na hilo Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kumpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kwa utendaji kazi wake katika kuisemea Serikali.
  • “Dkt. Abbasi umefanya kazi nzuri sana kwa kuisemea vizuri Serikali, nakupongeza sana kwa kuteuliwa  kuwa Katibu Mkuu hivyo utaendelea kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali hii mpaka atakapopatikana mtu mwingine “ amesema Rais Magufuli
  • Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma amemshukuru Rais Magufuli kwa kujaza safu na kuteua Viongozi   katika mahakama hivyo kwenda kurahisisha upatikanaji wa huduma.
  • “Nashukuru Rais magufuli  kwa kuendelea kujaza safu za mahakama, umetupatia viongozi ambao wana weledi wa kazi hii ya mahakama, hivyo nina amini kabisa tunaenda kufanya kazi a kuwatumikia watanzania” amesema Jaji Mkuu
  • Miongoni mwa walioapishwa leo na Rais Magufuli  ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo  Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wizara ya Nishati, Bi Zena Ahmed Said, katibu Mkuu Wizara ya Viwanda  Riziki Shemdoe, Katibu Mkuu wizara ya mambo ya ndani  ya Nchi Christopher  Kadilo, Katibu Mkuu  wizara ya Ardhi Bi Marry Gaspar  Makondo.
  • Wengine walioapishwa leo na Rais Magufuli  ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Steven Mhoja Mashauri,  Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Emmanuel  Mpawe Kukube, Naibu katibu Mkuu  wizara ya nishati  Leonard Robert Masanya.
  • Kwa upande kwa Mahakama Viongozi walioapishwa ni Msajili Mkuu wa mahakama ya Tanzania Wilbert Chuma, Msajili wa Mahakama ya Rufani Kelvin David, pamoja na Kamishna wa Magereza  Brigedia Jenerali Suleiman Mzee na Kamishna wa Jeshi la zima moto na uokoaji  John Wiliam.Na Eric Msuya – MAELEZO
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *