WAZIRI UMMY AKAGUA JNIA TERMINAL 3 UTAYARI WATUMISHI WA AFYA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

  • Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameridhishwa na hali ya ukaguzi wa abiria wanaoingia nchini katika uwanja wa ndege wa Kimataifa cha Julius Nyerere(JNIA) jengo la tatu la abiria-TB3 dhidi ya homa kali ya mafua inayoenezwa na virusi vya Corona.
  • Awali akiwa uwanjani hapo aliweza kutembelea kujionea maeneo mbali mbali ya utayari kwa watoa huduma ya afya ikiwemo chumba maalum cha kuwekwa mshukiwa pamoja na maeneo ya wanapoingilia wasafiri kutoka nje ya nchi.
  • “Nimekuja kuangalia kama kweli ukaguzi wa wasafiri unafanyika.
    Pili kuangalia kama wasafiri hao ambao wanaoingia tunapata taarifa zao zote kama wanatoka wapi na wanakuja kufanya nini na wanakaa muda gani.
1-01
Mmoja wa watumishi wa Afya akikagua joto la mwili kudhibiti homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona, kwa abiria uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jengo la tatu la abiria-TB3.
  • Pia nimetembelea kuona chumba cha kumuweka mshukiwa “nimekiona lakini nimetoa angalizo warekebishe sehemu ya choo kwa ajili ya kutenga sehemu ya choo kwa upande wa mwanaume na mwanamke.” Alisema Ummy Mwalimu.
  • Pia alipongeza hali ya ukaguzi uwanjani hapo inayofanywa na timu ya watumishi wa afya.
  • ” kwa ujumla hali ya ukaguzi wa wasafiri inaendelea vizuri na nimeridhika hali iliyopo lakini nataka kukiri tunahitaji kuongeza watumishi.
  • Hapa tuna mashine mbili hapa juu na chini pia imefungwa jengo la kwanza na la pili ”terminal 1, 2′.
  • Kikubwa tunawashukuru Mamlaka ya viwanja vya ndege ambao wapo hapa pia wanasimamia viwanja hivi kwa kushirikiana na timu yangu ya afya na mipakani.” Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
1
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa maagizo kwa maafisa afya wa uwanja wa ndege kuongeza eneo la maliwato kwa wanawake na wanaume kwenye chumba maalum cha wahukiwa wa virusi vya Corona katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jengo la tatu la abiria-TB3 
  • Aidha, amewataka kuhakikisha fomu za abiria wanaoingia kujazia ndani ya ndege ili kuondoa msongamano wanaopata baada ya kushuka.
  • “Nashauri fomu zote za kufuatilia hali ya virusi vya Corona zinajaziwa ndani ya ndege, wahakikishe fomu hizi zinajaziwa ndani ya ndege na wakitoka tu hapa wanaziwakilisha” alisema Ummy Mwalimu.
  • Hata hivyo alisema kwa sasa hali ya viwanja vya ndege na mipakani ipo salama na hakuna mshukiwa aliyepatikana na wote wanaoingia wapo chini ya joto 37.
  • “Watu ambao wanapimwa wapo vizuri. Lakini naomba nitoe angalizo. Unaweza kupimwa lakini usioneshe dalili za virusi hivi vya Corona. Nitoe wito kwa watanzania kama utaona hizi dalili ambazo tumezitoa usisite kwenda kituo cha afya kupata uchunguzi.
3-01
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akishudia abiria kutoka nje ya nchi wakipita katika eneo hilo la ukaguzi dhidi ya virusi vya Corona katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jengo la tatu la abiria-TB3
  • Unaweza kupita ukawa salama maana virusi hivi vinaweza kukaa hadi siku 14 bila kuonesha dalili hivyo kuna namba zetu tumeweka endapo utaona dalili zote tupige simu”. Alisisitiza Waziri Ummy.
  • Waziri Ummy Mwalimu alitoa angalizo kwa abiria wote wanaoingia nchini wakiwa na ‘mask’ zilizotumika kuwekwa eneo maalum ili kuzuia ugonjwa huo.
  • “Abiria wanakaa na mask kwenye ndege zaidi ya masaa nane. Naagiza tuweke eneo maalum na zikateketezwe kufuatana na muongozo.
    Naagiza muweke maelezo ya ‘tupa mask yako hapa’ ili kudhibiti ugonjwa huu ” alimalizia Waziri Ummy Mwalimu.
  • Kwa upande wake kaimu meneja wa jengo hilo la JB3, Mhandisi Bryton Komba alisema kwa sasa wanaendelea kufanya kazi ikiwemo kuangalia namna viwanja vingine wanavyokabiliana na virusi hivyo huku pia wakipokea agizo la Waziri wa afya la abiria kujazia fomu ndani ya ndege.
  • “Sisi kama watendaji tunapokea maagizo yote na tutawapeleka wadau tunaofanya nao kazi.
  • “Lakini pia tutaangalia vyumba muhimu vilivyohitajika na Waziri na tutawapatia na vitu vingine vinaendelea safi na mashine zote zinafanya kazi”. Alisema Mhandisi Komba.
  • Ugonjwa wa homa kali ya mapafu umesambaa nchi zaidi ya 20 duniani na kusababisha vifo zaidi 360. NA ANDREW CHALE
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *