WAKAZI WA PEMBEZONI MWA BAHARI WAELIMISHWA ATHARI ZA MAGENDO

  • Wakazi na wafanyabiashara waishio pembezoni mwa fukwe za Bahari ya Hindi katika kata za Somangila, Kimbiji na Pemba Mnazi zilizopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wameelimishwa kuhusu athari za magendo yanayopitishwa kinyume na sheria katika maeneo hayo.
  • Elimu hiyo imetolewa wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo inafanyika maeneo mbalimbali katika mikoa ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na Lindi.
1-01
Afisa Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Julieth Kidemi akiwaelimisha wakazi wa Mbuyuni kata ya Kimbiji wilayani Kigamboni kuhusu madhara mbalimbali yatokanayo na biashara za magendo wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi. Kampeni hii imeanza kufanyika tarehe 3 na itamalizika tarehe 11 Februari, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na Lindi.
2-01
Afisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ernest Mngube akiwaelimisha wakazi wa kata ya Kimbiji wilayani Kigamboni kuhusu madhara mbalimbali yatokanayo na biashara za magendo wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi. Kampeni hii imeanza kufanyika tarehe 3 na itamalizika tarehe 11 Februari, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na Lindi
  • Akizungumza na wakazi hao katika maeneo ya Buyuni na Kimbiji wilayani Kigamboni, Afisa Kodi Mkuu Rose Mahendeka kutoka mamlaka hiyo, amewaambia wakazi hao kuhakikisha wanatoa taarifa pindi wanapoona bidhaa za magendo ikiwa ni pamoja na kuepuka kutumia bidhaa hizo kwani zinaweza kuwa na madhara kwa afya zao.
  • “Ndugu zangu athari za magendo siyo tu kukwepa kodi ya serikali, lakini pia bidhaa hizo zinazopita katika njia zisizo rasmi, zinakuwa hazijathibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) na hivyo zinaweza kuwaletea madhara kiafya,” alisema Mahendeka.
4-01
Mmoja wa wakazi wa Mbuyuni kata ya Kimbiji wilayani Kigamboni akitoa maoni yake wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kampeni hii imeanza kufanyika tarehe 3 na itamalizika tarehe 11 Februari, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na Lindi.
  • Naye, Afisa Forodha kutoka TRA Ernest Mngube, amewaasa wafanyabiashara wanaojishughulisha na biashara za magendo kuacha tabia hiyo mara moja kwani wakibainika licha ya kuchukuliwa hatua za kisheria, watataifishiwa bidhaa zao ikiwa ni pamoja na vifaa vilivyotumika kubeba au kuhifadhi bidhaa hizo.
  • “Ni muhimu wafanyabiashara mtambue kwamba kupitisha bidhaa katika njia zisizo rasmi ni kinyume na sheria na mkibainika siyo tu mtachuliwa hatua kwa mujibu wa sheria bali bidhaa zenu zitataifishwa pamoja na vifaa kama gari, pikipiki, mashua zinazotumika bidhaa hizo na hata majengo yatakayokutwa yamehifadhi magendo hayo,” aliwaasa Mngube.
5-01
Wakazi wa kata ya Kimbiji wilayani Kigamboni wakimsikiliza kwa makini Afisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ernest Mngube (hayupo pichani) wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kampeni hii imeanza kufanyika tarehe 3 na itamalizika tarehe 11 Februari, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na Lindi.
  • Mgumbe amezitaja namba ambazo wananchi wanaweza kutoa taarifa kila wanapoona biashara za magengo katika maeneo yao ambazo ni 0746 23 24 91, 0800 75 00 75, 0800 78 00 78 au kutuma ujumbe wa whatsapp kwenda namba 0744 23 33 33 au kutuma barua pepe kwenda hu****@tr*.tz.  
  • Kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi imeanza kufanyika tarehe 3 na itamalizika tarehe 11 Februari, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na Lindi ikiwa na lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla madhara mbalimbali yatokanayo magendo hayo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SEKTA YA AFYA NCHINI KUNUFAIKA NA MSAADA WA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 600 KUTOKA GLOBAL FUND

Serikali ya Tanzania itanufaika na msaada wa dola za Marekani milioni 600 zitakazotolewa na Taasisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *