- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi (Kanali) Wilbert Augustine Ibuge kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
- Uteuzi wa Balozi Ibuge unaanza leo tarehe 06 Februari, 2020.
- Kabla ya uteuzi huo Balozi Ibuge alikuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
- Balozi Ibuge anachukua nafasi ya Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe ambaye amehamishwa wizara kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
- Dkt. Mnyepe anachukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye amestaafu.
- Uteuzi wa Mkuu wa Itifaki utafanywa baadaye na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Ibuge itatangazwa baadaye.
Tags KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Rais Rais Live WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO AFRIKA MASHARIKI Ziara za Rais Magufuli
Unaweza kuangalia pia
LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …