WANANCHI WANA WAJIBU WA KUEJIEPUSHA NA VITENDO VYOTE VINAVYOKWENDA KINYUME NA SHERIA NA KANUNI ZILIZOWEKWA NA (ZEC) NA (NEC) – RAIS DKT SHEIN

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi kuheshimu kazi, majukumu na maamuzi ya Tume za Uchaguzi nchini, kwa kuzingatia kuwa taasisi hizo zimeundwa kwa mujibu sheria na Katiba za nchi.

A-01

  • Dk. Shein amesema hayo katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul wakil Kikwajuni mjini hapa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria Zanzibar.
  • Alisema kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha anaheshimu kazi za vyombo hivyo katika uendeshaji na utoaji wa maamuzi katika masuala yote yanayohusu uchaguzi wa Zanzibar na ule wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Alisema wananchi wana wajibu wa kuejiepusha na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na sheria na kanuni zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) pamoja na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (NEC).

B-01

  • Alisema ni vyema kuhakikisha kwamba kila mwenye sifa na haki ya kushiriki katika uchaguzi huo, anafanya hivyo kwa kuelewa kuwa huo ni msingi muhimu wa kudumisha utawala bora na Demokrasia.
  • Aidha, alizitaka taasisi zinazoshughulikia masuala ya uchaguzi pamoja na usalama wa wananchi kufahamu wajibu walionao na kutekeleza majukumu yao ipasavyo, akibainisha umuhimu wa usalama wa nchi kuwa ndio lengo la Serikali.
Ad

Unaweza kuangalia pia

BALOZI SEIF: JUKUMU LA WATOTO WA SASA NI KUSOMA KWA BIDII ILI KUENDELEZA DHANA YA MAPINDUZI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Watanzania wanapoadhimisha Miaka …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *