- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewaapisha viongozi mbali mbali kushika nyadhifa baada ya kuwateuwa hivi karibuni.
- Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu mjini Unguja na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali, Dk. Shein amemuapisha Khatib Mwadini Khatibu kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ame Burhan Shadhil kuwa Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali.
- Miongoni mwa waliohudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Abdulhamid Yahya Mzee, Mawaziri, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Washauri wa Rais pamoja na watendaji mbali mbali.
Tags MAPINDUZI YA ZANZIBAR Rais Wa Zanzibar SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Unaweza kuangalia pia
BALOZI SEIF: JUKUMU LA WATOTO WA SASA NI KUSOMA KWA BIDII ILI KUENDELEZA DHANA YA MAPINDUZI
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Watanzania wanapoadhimisha Miaka …