DKT. YONAZI: TPC CHANGAMKIENI KILA FURSA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi amelitaka Shirika la Posta Tanzania kuchangamkia kila fursa inayotokea katika biashara na kuongeza ubunifu wa biashara hizo.

Ameyasema hayo leo Februari 14, 2021 katika kikao cha Menejimenti ya Shirika la Posta wakati alipokuwa akitoa semina ya mafunzo ya kibiashara na ubunifu kwa Viongozi wa Shirika hilo, jijini Dodoma.

Ad
Meneja Mkoa Tanga wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Walter Mariki akielezea namna ambavyo Mkoa wake umeona fursa katika kukuza biashara za Shirika.

Kikao hicho ambacho kilifunguliwa jana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) katika Ukumbi wa Mikutano Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, kilihusisha Viongozi wa Shirika la Posta nchini ambapo kila Kiongozi wa Mkoa alitoa wasilisho kulingana na Mkoa wake.

“Mfike mahali mpaka watu wajiulize hili ni Shirika la Posta au Shirika la wabunifu”, alisema Dkt. Yonazi.

Naibu Katibu Mkuu huyo aliitaka Idara ya Masoko kuongeza ubunifu na kuona fursa za kibiashara katika kila eneo ambalo Shirika linaona litapata faida.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Ndg. Waziri Kindamba akizungumza katika semina ya Menejimenti na Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) jijini Dodoma.

Aidha, Dkt. Yonazi amesema mbali na fursa za masoko, Shirika lina kada mbalimbali za kiutendaji zikiwemo idara na vitengo vingine katika ngazi ya Makao Makuu na Mikoa, upande wa vyama vya wafanyakazi na kila mmoja kwa nafasi yake alete tija katika kila anachokifanya kwa Shirika.

“Nataka kila mmoja afikirie kazi yake kiutofauti, unafanya kitu gani kipya, unaongeza nini kwa Shirika”.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba ameongeza kuwa mikakati na mbinu mpya zitumike Katika kukuza biashara za kiposta nchini, amesema kuwa watumishi wa Shirika wawe mfano wa kuzitumia huduma za Shirika kwa manufaa mapana ya Shirika. Pia amelipongeza Shirika kwa kuendelea kuboresha muonekano wa ofisi, majengo na huduma zake “Branding”. Hata hivyo ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Shirika katika kutoa huduma kwa jamii.

Meneja Rasilimali watu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Emmanuel Lugomela akielezea namna ambavyo Shirika linatoa mafunzo kwa watendaji wake. Anayemskiliza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi.

“Biashara ni vita na mikakati mbalimbali na ni lazima mjipange, na wakati mwingine kuhakikisha kupitia mbinu za medani ili kuhakikisha Posta yetu haiwezi kuhujumiwa, kufanyiwa vitimbi wala wala kuharibiwa”.

Kwa upande wake Postamasta Mkuu,Bw. Hassan Mwang’ombe amemshukuru Naibu Katibu Mkuu Dkt. Jim Yonazi kuja kutoa semina hiyo kwa viongozi wa Shirika na ameahidi kutumia miongozo iliyotolewa katika semina hiyo kuleta manufaa kwa Shirika. Pia amemshukuru na kumuahidi Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Waziri Kindamba kuendelea kushirikiana katika kukuza biashara za Posta na Mawasiliano nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Ndg. Waziri Kindamba akizungumza katika semina ya Menejimenti na Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) jijini Dodoma

Na Loema Joseph, TPC

“Nitoe shukrani zangu kwa kuleta muongozo utakaoleta matunda ndani ya Shirika, sasa mimi na wenzangu twende sawasawa na tulivyoelekezwa na tuone fursa zinazokuja mbele yetu kwa kulikuza Shirika”.

“Nikushukuru pia ndugu yangu Kindamba kwa kuja leo, sisi ni familia moja tuendelee kushirikiana na kwa kufanya hivyo tutaendelea kutoa huduma zenye tija kwa jamii”.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *