LUTEN JENERALI YACOUB AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MRADI WA KILIMO CHA MPUNGA KATIKA KIKOSI CHA JESHI LA KUJENGA TAIFA CHITA

Na. Sajini Mbwana Khalfan

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Yacoub Mohamed amefanya ziara ya kikazi na kutembelea mradi mkubwa wa kimkakati wa kilimo cha Mpunga katika kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa Chita, Wilayani Kilombero mkoani Morogoro tarehe 12 Februari 2021. Mradi huo unaogharimu shilingi Bilioni nne za kitanzania ni mkakati wa makusudi wa kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua.

Ad

Aidha, mradi huo ukikamilika unategemewa kuwa na jumla ya ekari 12000 ambapo hadi sasa ekari 2500 zimeshalimwa mpunga. Mradi huo utakuwa ndio mradi mkubwa hapa nchini wa kilimo cha Mpunga kwa njia ya umwagiliaji wenye lengo la kuongeza uzalishaji wa mchele nchini.

Luteni Jenerali Mohamed alilipongeza Jeshi la Kujenga Taifa kwa kubuni mradi huo wenye lengo la kuliletea Jeshi na Taifa tija zaidi.

Akiongea na Maafisa na Askari wa Kikosi hicho, Mnadhimu Mkuu alisisitiza nidhamu na weledi kazini na kudumisha ushirikiano uliopo wa vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kulinda Taifa.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *