WAZIRI UMMY MWALIMU AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA WFP

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu hii leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah Gordon – Gibson katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao wamekubaliana kushirikiana katika jitihada za kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na uharibifu mazingira nchini kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa chakula.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Bi. Sarah Gordon – Gibson akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *