PROF. KITILA AKUTANA NA WAAGIZAJI NA WAZALISHAJI MAFUTA YA KULA NCHINI

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amekutana na waagizaji na wazalishaji mafuta ya kula nchini ili kujua sababu na changamoto zinazosababisha kupanda kwa bei ya mafuta ya kula na kuweka mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kukabiliana na uhaba wa mafuta ya kula nchini

Waziri Prof. Mkumbo ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah na kukutana na wadau hao Mei 09,2021 Jijini Dar es salaam kufuatia bei ya mafuta ya kula kupanda katika maeneo mengi hapa nchini kwa kipindi hiki ambacho viwanda vya ndani havizalishi mafuta ya kutosha kutokana na upungufu wa malighafi.

“Mkatano wangu umelenga kusikiliza changamoto zinazosababisha mafuta ya kula kupanda bei katika masoko, tunafahamu kwamba kutokana na upungufu wa malighafi, viwanda vyetu vya ndani vya alizeti haviwezi kuzalisha kwa kiwango ambacho kinakidhi mahitaji ya ndani, nchi nzima inahitaji tani 570,000 na sisi tuna uwezo wa kuzalisha tani 210,000 peke yake, ili kufidia upungufu huu tunaagiza nje” ameeleza PRof.Mkumbo

Ad
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo


Waziri Prof. Mkumbo ametaja changamoto kubwa zinazosababisha kupanda kwa bei ya mafuta ambapo ameeleza kuwa bei ya mafuta ya mawese katika soko la Dunia imepanda bei, mwaka jana katika soko la Dunia walikuwa wanauza dola 600 kwa tani moja lakini kwa sasa wanauza dola 1200 kwa tani ambayo ni mara mbili ya bei ya mwaka jana, sababu nyingine kwa sasa waagizaji wanaagiza mafuta yaliyochakatwa kutoka nje kwa maana viwanda vitatu vikumbwa ya hapa nchini havifanyi kazi kwa sababu kulitokea mabadiliko ya kodi kipindi cha nyuma, waagizaji walikuwa wakiagiza mafuta yaliyochakatwa na wanaeeleza kuwa ni mafuta ghafi, serikali ili kudhibiti na kulinda viwanda vya ndani iliongeza kodi mpaka 35% ya uingizaji ya mafuta yaliyochakatwa.


Aidha, Waziri Prof. Mkumbo ameeleza kuwa kuanzia mwezi huu wa tano hadi mwezi saba kuna mavuno makubwa ya alizeti ambayo yatasaidia kupatika malighafi kwa viwanda vya alizeti na hivyo uzalishaji wa mafuta utaongezeka ambao utasaidi bei ya mafuta kushuka huku akieleaza namna Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ilivyojipanga kuwekeza katika utafiti wa kupata mbegu bora ya zao la alizeti na michikichi

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *