TANZANIA YASISITIZA KUWA BADO NI MWANACHAMA WA MAHAKAMA YA AFRIKA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU NA WATU

Tanzania imesema bado ni mwanachama hai wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na kwamba itaendelea kushirikiana na Mahakama hiyo pamoja na Taasisi nyingine za Utawala bora na haki za binadamu kuhakikisha haki za kila Mtanzania zinalindwa na kutetewa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Or’e na kuitumia fursa hiyo kufafanua hatma ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mahakama hiyo BALOZI MULAMULA

Ad

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Or’e amesema mahusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mahakama hiyo ni mzuri na kwamba katika mazungumzo yao moja ya jambo ambalo wamelitilia mkazo ni kuhusu kujenga majengo ya kudumu ya makao makuu ya mahakama hiyo Arusha nchini Tanzania…..Jaji  Sylvain Or’e

Katika hatua nyingine Balozi Mulamula amekutana na ujumbe wa Mtandao wa Taasisi ya za Kitaifa za Haki za Binadamu yaani Network of African National Human Rights Institutions ukioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo Bw. Gilbert Sebihogo,ambao uko hapa nchini kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa tamko la Marrakesh lililopitishwa 2018 kwa dhumuni la kulinda haki za watetezi wa Haki za Binadamu ili kukuza na kutetea haki za binadamu ambapo wameeleza kuridhishwa na mazingira yaliyopo hapa nchini.

Pembeni na mikutano hiyo Balozi Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Shalini Bahuguna Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuboresha huduma kwa watoto pamoja na kukabiliana na utapiamlo kwa watoto.   

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *