BODI YA MAZAO MCHANGANYIKO (CPB) YAASWA KUYAONGEZEA THAMANI MAZAO NCHINI

Waziri wa Kilimo nchini Mhe. Profesa Adolf Mkenda akipokea maelezo ya bidhaa itokanayo na zao la alizeti wakati wa sherehe ya kuzindua viwanda vya uchakataji mazao jijini Dodoma Jumatano iliyopita.

Bodi ya Mazao Mchanganyiko (CPB) nchini imeaswa kufanya jitihada za ziada katika kuyaongezea thamani mazao ili kuweza kushindana na soko la nchi za nje.

Hayo yalisemwa na waziri wa kilimo Mhe. Profesa Adolf Mkenda wakati akizindua viwanda vya bodi hiyo ya mazao mchanganyiko vilivyozinduliwa mnamo Jumatano iliyopita katika makao makuu ya Tanzania jijini Dodoma.

Ad

Profesa Mkenda aliitaka bodi hiyo na sekta binafsi zinazojihusisha na uchakataji wa mazao nchini kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao ili kuweza kuyapeleka kuuza nchi za nje.

Alisema kuwa ni vyema bodi hiyo ikaangalia ni namna inaweza kushirikiana na wakulima katika kuyaongezea thamani mazao.

“Nyie bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko mkisaidia na sekta binafsi mnaweza kutusaidia kuhakikisha mazao yetu yanaongezewa thamani,” alisema Profesa Mkenda.

Pia alitoa wito kwa bodi hiyo kuhakikisha inaingia mikataba na wakulima wenye mashamba makubwa nchini ili waweze kulima alizeti ya kutosha.

Naye Mkurugenzi wa bodi hiyo Bw. Anselm Moshi alisema kuwa kiwanda hicho cha alizeti kinauwezo wa kuchakata tani 40 kwa siku kutokana na ugumu wa upatikanaji wa malighafi.

Waziri wa Kilimo nchini Mhe. Profesa Adolf Mkenda (wapili kushoto) akishirikiana na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde, Mkurugenzi wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko (CPB) Dkt. Anselm Moshi na viongozi wengineo kuzindua viwanda vya uchakataji mazao jijini Dodoma Jumatano iliyopita.

“Kwa kuona hitaji la kuwa na mafuta yenye ubora, maana kuna mafuta mengi ya alizeti yanayochakatwa mitaani ambayo hayana ubora unaotakiwa, na hivyo viwanda hivi vitakuwa ni suluhisho la changamoto hiyo ya ubora,” alisema Bw. Moshi.

Aidha, naye Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema kuwa viwanda hivyo vitakuwa mkombozi kwa wakulima nchini.

“Zaidi ya watu 6500 watanufaika na viwanda hivi na hasa tukiongeza utaratibu wa kuwapa mikataba wakulima wetu wakawa ni wazambazaji wakuu wa malighafi tutakuwa pia tumeisaidia sana serikali katika kupunguza tatizo la ajira nchini,” alisema Mhe. Mavunde.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *