DKT. ANNA MAKAKALA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA UHAMIAJI MAKAO MAKUU DODOMA



Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini CGI Dkt. Anna Makakala ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la Uhamiaji Makao Makuu linaloendelea kujengwa Jijini Dodoma chini ya kampuni ya ujenzi ya SUMAJKT.

CGI Dkt. Makakala ameyasema hayo mapema leo hii alipokutana na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajab Mabele katika eneo la ujenzi na kuwataka SUMAJKT Wanaotekeleza mradi huo kuongeza juhudi na kasi ili kumaliza ujenzi huo kwa wakati.

Aidha ameipongeza SUMAJKT Kwa kuendelea kujenga jengo hilo kwa viwango na ubora unaotakiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele alimhakikishia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwamba Wataendelea kutekeleza ujenzi huo kwa Uhodari na weledi wa hali ya juu ili kukidhi ubora na viwango tarajiwa kwa manufaaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Meja Jenerali Mabele ameongeza nguvu ya wataalamu wengine wa ujenzi ili kuongeza ufanisi na kasi ya kumaliza jengo hilo kwa wakati.

Ujenzi wa jengo la Uhamiaji makao makuu Dodoma unatarajiwa kuwa na ghorofa nane kwenda juu na kukamilika mwaka 2022.

Maendeleo haya ya ujenzi wa jengo la ofisi ya makao makuu ya Uhamiaji Dodoma yanatokana na mafanikio ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuendelea kutoa fedha za ujenzi huo kwa wakati.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *