Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Septemba 7, 2021 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa wa kwanza wa Afrika na Umoja wa Nchi za “Carribbean”(Africa – CARRICOM Summit) uliofanyika kwa njia ya mtandao.
Akizungumza katika mkutano huo, Makamu wa Rais amesema nchi za afrika na za “ Carribean” zinafanana katika katika masuala mbalimbali hasa katika nia ya kuhitaji maendeleo ya haraka hivyo kuwepo na ushirikiano baina nchi hizo kutaongeza kasi ya maendeleo pamoja na kuwa na sauti ya pamoja kwa manufaa ya mataifa yote ndani ya umoja huo.
Makamu wa Rais amesema Tanzania inaunga mkono mapendekezo ya kuwepo kwa siku maalum ya umoja huo pamoja kuziasa nchi washiriki wa mkutano huo kuendelea kutoa msukumo wa kupatikana kwa chanjo kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona katika nchi zinazoendelea zenye uhitaji mkubwa wa chanjo hiyo.
Mkutano huo umejadili ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Bluu, Afya, Teknolojia Mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kudhibiti ugojwa wa Corona.
Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Carribean.