WAZIRI MKENDA AZITAKA BODI NA TAASISI KUHAMASISHA TIJA NA UZALISHAJI WA MAZAO

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) amempongeza Katibu Mkuu wa wizara ya Kilimo Ndg Andrew Massawe kwa kuzisimamia kwa weledi mkubwa Bodi na Taasisi zilizo chini yake hivyo kuendeleza uwajibikaji kuhakikisha kuwa sekta ya kilimo inaendelea kuimarika.

Ad

Amesema kuwa wananchi wana imani kubwa na Wizara ya kilimo hivyo kuna kila sababu ya kuongeza weledi katika uwajibikaji ikiwa ni pamoja na kuwasajili wakulima ili kuwatambua jambo litakaloiwezesha serikali kuwatambua wakulima hao na kuweza kuwahudumia.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao cha kazi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wzara ya Kilimo, pamoja na Wakuu wa Bodi na Taasisi kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wzara ya Kilimo, pamoja na Wakuu wa Bodi na Taasisi kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma, leo tarehe 9 Septemba 2021.

Akizungumza kuhusu Tija na uzalishaji wa mazao nchini Waziri Mkenda amesema kuwa Kiwango cha uzalishaji na tija kwenye mazao mengi hapa nchini bado kipo chini. Kwa mfano, uzalishaji wa korosho kwa sasa ni wastani wa kilo 5 hadi 10 kwa mti ikilinganishwa na tija ya juu ya kilo 35 kwa mti inayoweza kufikiwa kulingana na viwango vya kitaalam.

Baadhi ya sababu zinazosababisha kuwepo kwa tija ndogo kwenye mazao ni pamoja na Matumizi madogo na yasiyokuwa sahihi ya pembejeo, Uwekezaji mdogo kwenye tafiti za kimaendeleo,Huduma duni za ugani, naKuyumba kwa masoko ya mazao kwenye baadhi ya misimu.

Amesema kuwa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau imeendelea na jitihada za kuongeza uzalishaji na tija katika mazao ya kimkakati ikiwemo korosho ili kuongeza kipato cha mkulima na taifa kwa ujumla.

Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wzara ya Kilimo, pamoja na Wakuu wa Bodi na Taasisi wakifuatilia kikao cha kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma, leo tarehe 9 Septemba 2021.

“Mfano kwenye zao la Pamba kwa sasa wanaendelea na kampeni kubwa ya kuongeza tija na uzalishaji kwa kumtumia Balozi wa Pamba Ndg Aggrey Mwanri ambapo wameanza kampeni hiyo mkoa wa Simiyu, Shinyanga na kwa sasa wataelekea Geita kabla ya kuelekea katika mikoa mingine” Amesisitiza Waziri Mkenda

Katika kikao kazi hicho Waziri Mkenda amempongeza Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe kwa usimamizi na uwajibikaji uliotatua muarobaini wa kadhia ya kuchelewa kwa viuatilifu na hatimaye kufanya juhudi kubwa k.uhakikisha viuatilifu vinafika kwa wakati kwa wakulima wa zao la korosho.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) ameitaka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko-CPB na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula-NFRA kuhakikisha kuwa inawafuata wateja wakati wa ununuzi wa nafaka ili kuwarahisishia huduma katika maeneo walipo.

Kuhusu zao la alizeti Mhe Bashe amesema kuwa serikali inaendelea na juhudi kubwa kuhakikisha kuwa mbegu za alizeti zinapatikana kwa wingi na kwa wakati.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *