PROF MKENDA ATAKA MIKAKATI UBANGUAJI KOROSHO KUFIKIA 60% IFIKAPO 2025

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda amewataka wabanguaji zao la korosho kuja na mikakati  itakayowezesha zoezi hilo kufikia asilimia 60 au 100 ifikapo mwaka 2025.

Ad

Waziri Mkenda ameyasema hayo mjini Mtwara wakati akizungumza na wadau wa ubanguaji Korosho kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapo.

Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati wa kikao cha wadau wa ubanguaji wa korosho kilichofanyika mkoani Mtwara, jana, kikiwa na lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wadau hao, Tarehe 20 Septemba 2021.

Amesema kuwa madhumuni ya kikao hicho ni kushauriana kujenga mwelekeo wa kuhakikisha kwamba adhma inafikiwa ya walau kwa kima cha chini kabisa asilimia 60 ya korosho ibanguliwe hapa nchini.

“Na hicho ni kima cha chini kabisa ikifika mwaka 2025 maana kima cha chini kabisa ni kwamba tukifika asilimia 100 tena ndio tutafurahi zaidi sasa kwa kasi ambayo tunakwenda nayo ni vizuri tukawa tunashauriana kwa maana 2025 ni kesho tuu,”.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga akielezea fursa zilizoko katika mkoa wake wakati wa kikao cha wadau wa ubanguaji wa korosho kilichofanyika mkoani Mtwara, jana, kikiwa na lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wadau hao, Tarehe 20 Septemba 2021.

Amesema kuwa kwa sasa ni asilimia 10 tu ya korosho inabanguliwa hapa nchini na ubora umeongezeka na ladha imekuwa nzuri zaidi Lakini linahitajika soko kubwa la nje kwa kuwa fedha nyingi zipo huko.

“Tukiweza kuwauzia wale sababu kipato na fedha zipo huko nyingi, wakulima watakuwa na fedha nyingi zaidi na kutakuwa na ajira za kutosha nchini hasa maeneo ya Mtwara na Lindi na Serikali itapata fedha,”.

Alibainisha ni changamoto inayotakuwa kufanyiwa kazi  kwa kushirikiana na wadau wote kwakuwa Serikali haiwezi kutekeleza yenyewe kwa kukaa ofisini.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akisisitiza juu ya umuhimu wa ushirikiano baina ya wadau wa ubanguaji wa korosho wakati wa kikao cha wadau hao kilichofanyika mkoani Mtwara, jana, kikiwa na lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wadau hao, Tarehe 20 Septemba 2021.

Naibu Waziri wa kilimo, Mhe Hussein Bashe amesema kuongeza thamani kwenye zao hilo ni jambo la msingi husuani kwenye ubanguaji.

Amesema zipo changamoto za riba kwenye zao hilo ambapo Rais ametoa Trilioni moja kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli za kiuchumi zitakazokopeshwa chini ya asilimia 10 na taasisi za fedha.

Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, Francis Alfred akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa ubanguaji wa korosho kilichofanyika mkoani Mtwara, jana, kikiwa na lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wadau hao, Tarehe 20 Septemba 2021.

Amesema changamoto wanayokabiliana nayo wabanguaji ni mitaji kwamba kiwanda kina uwezo wa kuchakata tani 10 kwa siku maana yake kwa mwezi ni tani 300 hivyo ili kufanye kazi mwaka mzima kinahitaji zaidi ya tani 3,600.

Amebainisha kuwa zipo changamoto za kisera ambazo zimeshaanza kufanyiwa kazi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za fedha ili wabangue korosho kwa kiasi kikubwa.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *