RAIS SAMIA MGENI RASMI TAMASHA LA MICHEZO LA WANAWAKE LA TANZANITE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua Tamasha la Kwanza la Michezo la Wanawake la Tanzanite litakalofanyika katika viwanja vya Uhuru na Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kuanzia Septemba 16 hadi 18, 2021 huku uzinduzi rasmi ukifanyika Jumamosi, Septemba 18. 

Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi


Katibu Mkuu anayesimamia sekta za Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi,  ameyasema hayo leo Septemba 15, 2021 alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. 

Ad


“Toka aingie madarakani Rais Samia ameonesha nia ya dhati ya kuinua michezo kwa wanawake hivyo amekubali kuja kuzindua Tamasha hili ambalo litaanza tarehe 16-18 Septemba, 2021’” Amefafanua Dkt. Abbasi.


Amesema Tamasha hilo la kihistoria limesheheni michezo mbalimbali ikiwemo Riadha, ndondi, soka, netiboli, mpira wa kikapu, wavu, karate, Makomando wa kike, kuvuta kamba, rede na mingine mingi.


“Katika kunogesha Tamasha hilo kutakuwepo wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya huku asilimia zaidi ya 98 wakiwa ni wakike ambao nao wataonesha uwezo wao,” alisema Dkt. Abbasi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan, Mwana Mfalme Bi. Zahra Aga Khan

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *