MWENYEKITI WA BODI YA TAASISI YA GWPSA – AFRICA RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE ASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MAJI

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Senegal Macky Sall, Ikulu ya Senegal,

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa Wadhifa wake wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayojishughulisha na Masuala ya Maji Barani Afrika (Global Water Partnership – Southern Africa and Africa Coordination Unit – (GWPSA – Africa)) ameshiriki katika Mkutano wa Kimataifa Kuhusu Maji (World Water Forum) Mjini Dakar nchini Senegal.

Akiwa Dakar, Rais Mstaafu amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Macky Sall, Rais wa Jamhuri ya Senegal, Ikulu ya Senegal, ambapo wameongelea mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa maji safi, salama na toshelevu Barani Afrika.

Ad
Ad

Unaweza kuangalia pia

Nafasi ya Katiba ya Tanzania katika Kuhamasisha Matumizi Mbadala ya Nishati kwa Maendeleo Endelevu na Afya Bora.

Katiba ya Tanzania inafafanua vipengele muhimu vinavyohusiana na matumizi mbadala wa nishati kama njia ya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *