Matokeo ChanyA+

Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+.

SERIKALI KUWEZESHA WAKALA WA MBEGU ZA KILIMO (ASA) KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU BORA NA KUIMARISHA SOKO LA ZAO LA NAZI

Upatikanaji wa mbegu bora zikiwemo za mahindi ngano, maharage, mpunga, soya, alizeti, mtama, ufuta, viazi mviringo na mbegu za mazao ya bustani kwa msimu wa 2018/19 ulifikia tani 49,040 kati ya hizo tani 38,507 sawa na asilimia 78.6 zilizalishwa nchini na tani 8,361 sawa na asilimia 17 ziliagizwa nje ya …

Soma zaidi »

SERIKALI YAKAMILISHA MCHAKATO WA KUWASOMESHA WATAALAM 100 WA KILIMO ISRAEL

Serikali imekamilisha zoezi la kuwapeleka wataalam 100 wa kilimo nchini Israel kujifunza mbinu bora na teknolojia za kisasa za kuendeleza kilimo cha umwagiliaji nchini. Akiongea na wataalam hao wakati wa hafla ya kuwaaga jana jioni, Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika …

Soma zaidi »

MKANDARASI MRADI WA UMEME MTERA ATAKIWA KUMALIZA KAZI OKTOBA, 2019

Mkandarasi anayetekeleza mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Mtera, ameagizwa kumaliza kazi hiyo ifikapo tarehe 4 Oktoba mwaka huu ili kuwezesha vijiji takribani 70 katika mkoa wa Iringa na Dodoma kupata umeme wa uhakika kwani sasa wanapata umeme wenye nguvu dogo. Maagizo hayo yalitolewa na Waziri wa …

Soma zaidi »

BUNGE LA RIDHIA MKATABA WA MINAMATA KUHUSU ZEBAKI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amesema inakadiriwa kuwa asilimia 25 hadi 33 ya wachimbaji wadogo wa dhahabu hapa nchini, wameathiriwa na Zebaki kwa kupata magonjwa yakiwemo yale ya mifumo ya neva za fahamu, uzazi, upumuaji, figo, moyo, na udhaifu wa mwili. …

Soma zaidi »

UJERUMANI YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BIL. 32.7 KUSAIDIA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KFW) imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 13, sawa na sh. bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama Tumaini la …

Soma zaidi »