Matokeo ChanyA+

Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+.

SERIKALI YAJIPANGA KUUNGANISHA GESI ASILIA MAJUMBANI NCHI NZIMA

Serikali imesema Mradi wa kuunganisha gesi asilia majumbani ni endelevu na utafanyika katika mikoa yote nchi nzima awamu kwa awamu. Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, alibainisha hayo jana, Mei 25, 2019 jijini Dodoma katika Semina ya Wabunge wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ambayo ililenga kuwajengea …

Soma zaidi »

MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI WAZINDULIWA

Serikali imezindua Mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa Vijiji, Wilaya na Mikoa itakayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ikiwa ni hatua nyingine katika utekelezaji wa mradi huo. Mpango huo umezinduliwa katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora tarehe …

Soma zaidi »

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA IKULU YA PRETORIA NCHINI AFRIKA KUSINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Mei, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa, Ikulu Jijini Pretoria. Katika Mazungumzo hayo, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Rais Ramaphosa kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu …

Soma zaidi »

MCHOME AKAGUA UTOAJI WA MSAADA WA KISHERIA MKOANI SINGIDA

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome atembelea mkoa wa Singida kukagua utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi. Prof Mchome yuko katika ziara ya ukaguzi wa huduma na maeneo yanayotolewa msaada wa kisheria ili kuona kama inaendana na matakwa ya Sheria ya Msaada wa Kisheria No …

Soma zaidi »

WABUNGE WA LINDI NA MTWARA WATOA HOJA KATIKA WARSHA KUHUSU MRADI WA GESI ASILIA ILIYOSINDIKWA (LNG)

Hoja  1. Fidia kwa wananchi Ufafanuzi wa Serikali Fidia ni haki, ni stahiki na ni jambo la kisheria. Kama Serikali, hatuwezi kulipindisha. Tunachofanya ni kujihakikishia kwamba watakaofidiwa ni wale tu wanaostahili kweli. Kutokana na umuhimu wa jambo hili, lazima lifanyike kwa umakini sana. Ipo hatari ya kulipa haraka-haraka, kisha wakajitokeza …

Soma zaidi »