Taarifa ya Habari

MRADI WA UJENZI WA MELI MPYA NA CHELEZO WASHIKA KASI

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi jana (Oktoba 31) alitembelea  mradi wa ujenzi wa meli ya kisasa ambayo ni meli kubwa kuliko zote katika Ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na ujenzi wa chelezo kwa ajili ya matengenezo na marekebisho ya meli …

Soma zaidi »

BODI YAWEKA KUSUDIO KUMFUTIA MKATABA MKANDARASI WA REA

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imeweka kusudio la kufuta mkataba mmojawapo wa mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Mtwara na sehemu ya Mkoa wa Tanga, ambaye ni muunganiko (JV) wa kampuni za Radi Services Ltd, Njarita Contractors Ltd & Aguila Contractors Ltd. Kusudio hilo liliwekwa bayana mbele ya waandishi …

Soma zaidi »

TANZANIA KUANZISHA KITUO CHA KIMATAIFA CHA USULUHISHI WA MIGOGORO YA KIBIASHARA

Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimekubaliana kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) hususani katika kusimamia mashauri katika …

Soma zaidi »

BODI YATOA TATHMINI KUHUSU UTEKELEZWAJI MIRADI YA UMEME VIJIJINI MOROGORO

Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Oktoba 25, mwaka huu ilikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Olesanare, taarifa ya tathmini kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo, baada ya ziara yao ya siku mbili. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Styden Rwebangila, …

Soma zaidi »

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WAPYA WA FINLAND, UMOJA WA ULAYA NA RWANDA

Rais Dkt. John  Magufuli amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini Mhe. Manfred Fanti, Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Riitta Swan na Balozi wa Rwanda hapa nchini Mhe. Mej. Jen. Charles Karamba, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Mhe. Rais Magufuli baada …

Soma zaidi »

WANANCHI WENGI WAJITOKEZA KUFANYIWA UCHUNGUZI SARATANI YA MATITI

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania-MEWATA- imefanya zoezi la uchunguzi wa awali wa saratani ya matiti bila malipo kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya ugonjwa huo na kuhamasisha jamii umuhimu wa kujichunguza mapema.  Zoezi la uchunguzi limefanyika kwa siku mbili ambapo kina mama …

Soma zaidi »