Taarifa ya Habari

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeidhinisha jumla ya Shilingi bilioni 55,175,163,302 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kwa Wizara ya Katiba na Taasisi zake. Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 47,283,566,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na mishahara na shilingi Bilioni 7,891,598,000 …

Soma zaidi »

SHIRIKA LA SUN FLOWER KUJENGA KIWANDA NCHINI

Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uzalishaji wa Kilimo cha Alizeti {Sun Flower} la Alemdar kutoka Nchini Uturuki limeonyesha nia ya kutaka kujenga kiwanda kitakachozalisha Bidhaa tofauti kwa kutumia malighafi ya Maua hayo katika azma ya kuitikia wito wa Serikali wa kuwa Nchi ya Viwanda katika kipindi kifupi kijacho. Ofisa Mkuu …

Soma zaidi »

WATUMISHI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WATAKIWA KUBORESHA ZAIDI MIFUMO YA UKUSANYAJI MAPATO YA SERIKALI

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji , amewataka  Watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato ya ndani na kupanua wigo wa walipakodi pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali. Dkt. Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza …

Soma zaidi »

SERIKALI YASHUSHA GHARAMA ZA URASIMISHAJI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuanzia sasa gharama za urasimishaji haitazidi shilingi 150,000 badala ya 250,000 iliyopangwa awali na makampuni yatakayoenda kinyume yatachukuliwa hatua ikiwemo kufutwa. Lukuvi alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Makampuni ya Upangaji na Upimaji yanayofanya kazi …

Soma zaidi »

WAZIRI KALEMANI ASISITIZA TAASISI ZA UMMA VIJIJINI ZIWEKEWE UMEME

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewaagiza wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchi nzima, kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha kuunganisha umeme kwa taasisi zote za umma zilizo katika maeneo yao. Alitoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti jana, Aprili 16, 2019 akiwa katika …

Soma zaidi »

JAPAN KUIPIGA JEKI TANZANIASHILINGI BILIONI 794 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa-JICA inakusudia kuipatia Tanzania mkopo nafuu pamoja na ruzuku wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 345 za Marekani, sawa na takriban shilingi bilioni 794, kwa ajili ya kutekeleza miradi mitatu ya maendeleo ikiwemo ukarabati wa barabara ya Arusha hadi Holili, …

Soma zaidi »