Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Ofisi yake baada ya kumaliza majukumu yao kwa siku ya kwanza katika Ofisi zao mpya zilizopo katika Mji wa Serikali.

OFISI YA WAZIRI MKUU YAHAMIA RASMI MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

KATIBU MKUU
Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akiwa anatekeleza majukumu yake katika Ofisi yake Mpya iliyopo katika Mji wa Serikali Kata ya Mtumba, Jijini Dodoma ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa tarehe 13 Aprili, 2019.
KATIBU MKUU
Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akizungumza na baadhi Wakuu wa Idara na Vitengo wakati alipofanya kikao cha kuwakaribisha katika ofisi zao mpya zilizopo katika Mji wa Serikali Aprili 15, 2019.
MKURUGENZI
Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Joseph Mramba (katikati) akieleza jambo kwa Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna (hayupo pichani) juu ya utayari wa kutekeleza majukumu yao wakati wa kikao hicho kilichofanyika Aprili 15, 2019 katika Mji wa Serikali, Jijini Dodoma.
AFISA
Afisa Mipango Miji wa Jiji la Dodoma, Bw. William Alfayo (wa tatu kutoka kulia) akiwaonesha baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waliombatana na Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi (wa pili kutoka kushoto) maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Balozi katika Mji huo.
KASSIM-5
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Madini, Bw. Msajigwa Kabigi (wa pili kutoka kulia) akimpa taarifa Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi (katikati) juu ya zoezi la kuamishia ofisi zao rasmi katika Mji huo wa Serikali uliopo Kata ya Mtumba, Jijini Dodoma
KASSIM-6
Muonekano wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) iliyopo katika Mji wa Serikali uliopo Kata ya Mtumba, Jijini Dodoma.
OFISI
Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Naibu waziri wa Madini iliyopo katika Mji wa Serikali alipotembelea Wizara hiyo ambayo tayari imekwisha hamia Mji wa Serikali.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *