WIZARA YA MAMBO YA NJE

MKUTANO WA USHIRIKIANO WA UCHUMI NA BIASHARA KATI YA AFRIKA NA CHINA UMEFANYIKA JIJINI JINHUA

Mkutano wa Ushirikiano wa Uchumi na Biashara kati ya Afrika na China umefanyika jijini Jinhua katika Jimbo la Zhejiang na kuhudhuriwa na Wanadiplomasia wa Nchi za Afrika, viongozi wa Serikali ya Jimbo la Zhejiang na Mji wa Jinhua pamoja na wafanyabiashara wa China na Afrika. Katika mkutano huo Naibu Katibu …

Soma zaidi »

TANZANIA IMETAJWA KAMA NCHI YA KIELELEZO CHA AMANI NA DEMOKRASIA KATIKA BARA LA AFRIKA

Norway yaitaja Tanzania kama kielelezo cha amani na demokrasia katika chaguzi Barani Afrika kutokana na mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu unavyofanyika kwa amani,utulivu na usawa kwa wagombea wa vyama vyote huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kusikiliza sera za wagombea. Balozi wa Norway nchini Tanzania Balozi Elisabeth Jacobsen ameyasema hayo …

Soma zaidi »

NCHI 15 ZARUHUSIWA KULETA WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU 2020

Balozi wa Umoja wa Ulaya Balozi Manfred Fanti akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam Nchi 15 kupitia Balozi zao hapa nchini zimeruhusiwa kuleta waangalizi wa Kimataifa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi …

Soma zaidi »

SADC NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAJADILI, KUBORESHA RASIMU ZA NYARAKA ZA KISERA NA KIMKAKATI

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ngazi ya Makatibu Wakuu wamekutana na kujadili rasimu ya mpango mkakati elekezi mpya wa maendeleo wa kanda (2020 – 2030) pamoja na rasimu ya dira ya SADC (2020 – 2050) kwa njia ya (Video Conference) jijini Dar …

Soma zaidi »

TANZANIA YACHUKUWA UENYEKITI WA NCHI 79 ZA OACPS NA KUELEZEA KIPAUMBELE CHAKE

Tanzania imesema itatumia kipindi chake cha uenyeketi wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific na Umoja wa nchi za Ulaya katika kusisitiza juu ya urejeshwaji wa rasilimali zilizoporwa katika nchi hizo nyakati za ukoloni,kuheshimu mamlaka ya nchi husika na urejeshwaji wa wahamiaji haramu kwa kuzingatia utu na haki za binadamu.Naibu …

Soma zaidi »

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO, KUKUZA MAENDELEO

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo endelevu.  Makubaliano hayo yamefanywa na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, wakati alipokutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge …

Soma zaidi »

PROF. KABUDI AKUTANA, KUMUAGA BALOZI WA IRELAND NCHINI TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, amekutana na kumuaga Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock ambaye amemaliza muda wake wa utumishi na amemtakia maisha mema na kumwambia kuwa ni matarajio yake kuwa atakuwa balozi mwema kwa Tanzania nchini Ireland na kwingineko duniani. …

Soma zaidi »

TANZANIA YAENDELEA KUZIOMBA TAASISI ZA FEDHA ZA KIMATAIFA KUSAMEHE MADENI NCHI ZINAZOENDELEA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuziomba taasisi za fedha za kimataifa pamoja na nchi za Jumuiya ya madola kufikiria kufuta kabisa madeni yaliyokopeshwa kwa nchi zinazoendelea ili fedha hizo ziweze kutumika kupambana na athari zilizotokana na Covid 19. Ombi hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje …

Soma zaidi »