Maktaba Kiungo: ELIMU YA MSINGI TANZANIA

MAONESHO YA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YAFANYIKA KWA MARA YA KWANZA

Na Lilian Lundo – Dodoma. Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mara ya kwanza limeandaa Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ambayo yamefanyika Jijini Dodoma tarehe 27 hadi 30 Mei, katika uwanja wa Jamhuri. …

Soma zaidi »

UPANUZI CHUO CHA UALIMU PATANDI KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA WALIMU WA ELIMU MAALUM

Serikali imekamilisha upanuzi wa Chuo cha Ualimu Patandi ili kukiongezea uwezo wa kudahili walimu wenye taaluma ya elimu maalum wanaohitajika nchini ili kupunguza changamoto ya walimu hao. Hayo yameelezwa leo Bungeni, Jijini Dodoma na Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akijibu swali la Mhe. Grace Victor Tendega Mbunge wa Viti Maalum kwa …

Soma zaidi »

MAKATIBU WAKUU WA HABARI NA ELIMU WAKUTANA KUJADILI SULUHU YA ENEO LA KIMILA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA.

Makatibu Wakuu wa Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi na Katibu Mkuu Wizara ya  Elimu , Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo pamoja na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Dkt. Masudi Senzia wamekutana na Viongozi wa Wazee wa Kimasai ili kupata suluhu la eneo la …

Soma zaidi »

LIVE:RAIS MAGUFULI AKIWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA MAKTABA YA CHUO CHA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST)

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli  anaendelea na ziara  ya kikazi mkoani mbeya ambapo leo ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa maktaba katika chuo kikuu cha Teknolojia Mbeya pamoja na kuzindua upanuzi wa Kiwanda cha Mbeya CEMENT. Katika uzinduzi huo wapo viongozi mbalimbali wa …

Soma zaidi »

URAFIKI WETU TANZANIA NA CHINA UNA FAIDA NA MAFANIKIO MAKUBWA – PROF. NDALICHAKO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, zimeadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia ulioasisiwa na Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mao Ze Dong, Rais wa kwanza wa  China. Akiongea katika maadhimisho …

Soma zaidi »

UTOAJI WA ELIMU BORA NI KIPAUMBELE CHA NCHI – WAZIRI MKUU MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema utoaji wa elimu bora kwa Watanzania ni moja ya vipaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo na kufikia malengo ya Milenia 2025, Elimu kwa wote (EFA) na Mkakati wa Kupambana na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA). Amesema ili kuweza kufanikisha malengo hayo wanahitaji sekta hiyo kuwa bora, …

Soma zaidi »

ZANZIBAR KUTOA USHIRIKIANO KWA SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Simai Mohamed Said amesema Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano kwa shirika la nguvu za atomiki Dunia  ili kukuza na kuimarisha teknolojia ya utumiaji wa mionzi. Ameyasema hayo katika mkutano wa pamoja na ujumbe wa shirika la Nguvu za Atomic Duniani (IAEA) kanda …

Soma zaidi »

SERIKALI IMEIMARISHA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA MATUMIZI SALAMA YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA NCHINI.

Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imefanikiwa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya  Teknolojia ya Nyuklia nchini.  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekenolojia Mheshimiwa William Ole Nasha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya Sayansi  na …

Soma zaidi »