Picha ikimuonyesha Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh William Ole Nasha akiwanna washiriki wa mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia kutoka katika nchi wanachama 49 wa Shirika la Nguvu za Atomiki duniani

SERIKALI IMEIMARISHA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA MATUMIZI SALAMA YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA NCHINI.

  • Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imefanikiwa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya  Teknolojia ya Nyuklia nchini.  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekenolojia Mheshimiwa William Ole Nasha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya Sayansi  na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi  46 wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki ( IAEA ) unaofanyika jijini Arusha.
ATOMIKI-1
Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Tekenolojia Mh William Ole Nasha akisalimiana na Naibu waziri anayeshughulikia mashirika ya nje nchini Liberia katika wizara ya Mambo ya nje Bi. Yaba Freeman Thompson ambaye pia ni mratibu wa mradi na mahiriki katika mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya sayansi na Tekenolojia ya Nyuklia kanda ya AFRIKA .
  • Naibu waziri Ole Nasha amesema  Shirika hilo linafadhili miradi mingi katika sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo sekta ya afya ambapo imewezesha kupatikana kwa  vifaa mbali mbali vya uchunguzi wa tiba na maradhi ya saratani ambavyo vimefungwa katika hospitali ya Rufaa  ya kanda ya ziwa Bugando  jijini Mwanza  na Hospitali ya Ocean Road  jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Tume
Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Profesa Lazaro Busagala akitoa neon la ukaribisho kwa wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi wanachama 49 wa Shirika la Nguvu za Atomiki la kimataifaIAEA)
  • Pamoja na vifaa vya uchunguzi katika hospitali hizo mbili, pia taasisi nyingine mbalimbali zimepata vifaa  vya maabara ambapo kwa ujumla wake vifaa vyote vina thamani ya kiasi cha shilingi  za Tanzania bilioni 6.2 na pia kutoa mafunzo kwa wataalamu katika eneo  la matumizi ya mionzi na Teknolojia ya Nyuklia mpango ambao uligharimu Shilingi za Tanzania Bilioni 3.3.
  • Mh Ole Nasha amelishukuru na kulipongeza shirika hilo kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa wanachama hususan kwa utaratibu wake wa kuwa na mikutano  inayowezesha kubadilishana uzoefu baina ya wanachama. Amewataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha wanafanya majadiliano yenye tija kwa lengo la kusaidia nchi zao kwenye udhibiti  na matumizi salama ya teknolojia ya nyukulia. “ majadiliano yenu yalenge katika kuhakikisha mionzi na teknoljia ya Nyuklia katika Afrika inatumika vizuri kwa maendeleo”.Alisema.
NAIBU WAZIRI ELIMU
Naibu waziri Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh William Ole Nasha wakati akifungua mkutano wa kimataifa unaohusisha waratibu wa miradi ya sayansi na teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi za kanda ya AFRIKA
  • Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Profesa Shaukat Abdulrazak amesema wataendeela kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia ya Nyukilia kwenye sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya , Kilimo,Mifugo,Maji  ,Viwanda na Ujenzi.
  • Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Nguzu za Atomiki Tanzania , Profesa Lazaro  Busagara amesema taasisis yake imeendelea udhibiti na kuwachukulia hatua za kuwafungia taasisi zinazokiuka taratibu za matumizi salama ya Mionzi na Teknolojia ya Nyuklia hapa nchini ikiwemo kutokuwa na leseni, kutokuwa na wafanyakazi wenye utaalamu wa matumizi ya mionzi na teknolojia ya Nyuklia na Mionzi.
NAIBU WAZIRI
Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh William Ole Nasha (Kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Shirika la nguvu za Atomiki Duniani Profesa Shaukat Abdulrazak kwenye mkutano wa kimataifa unahusisha nchi 49 za kanda ya AFRIKA.
  • Akitoa mfano wa Hospitali amesema  mwaka 2018 walifungia hospitali 112 zilizoshindwa kufuata masharti hayo, katika hizi tayari hospitali 40 zimekidhi na kufunguliwa huku hospitali 72 zikiwa bado zimefungiwa kutumia vifaa vinavyotumia mionzi .
  • Mkutano huo wa Siku tano utamalizika tarehe 15 , Machi  2019.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MWANAFUNZI WA MALANGALI AINGIA KUMI BORA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

#SisiTumeona SISI WATANZANIA TUNAWEZA Hivi sasa watoto wetu wanapata elimu bure bila malipo! ——————————— Matokeo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *