Maktaba Kiungo: WAZIRI WA NISHATI

TANZANIA NA ANGOLA ZAJADILI USHIRIKIANO KATIKA MAFUTA NA GESI

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amekutana na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Sandro De Oliveira na kufanya mazungumzo kuhusu  ushirikiano katika utafiti wa Mafuta na Gesi pamoja na ununuzi wa mafuta. Mazungumzo kuhusu ushirikiano huo yalifanyika tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, …

Soma zaidi »

BUNGE LARIDHIA MKATABA WA UANZISHWAJI USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WA NISHATI JUA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia Mkataba wa kuanzishwa kwa Ushirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (ISA), katika Mkutano wake wa Kumi na Saba, Novemba 14, 2019 Dodoma. Awali, akiwasilisha Azimio la Bunge kwa ajili ya kuridhia Mkataba huo, Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani alieleza kuwa …

Soma zaidi »

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA KUSAIDIA UJENZI WA MIRADI YA NISHATI TANZANIA

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kuendelea kuisadia Tanzania kutekeleza miradi yake mikubwa ya kimkakati hususan miundombinu ya Nishati na Barabara kwa kuendelea kuipatia mikopo yenye masharti nafuu ili kuharakisha maendeleo ya nchi. Ahadi hiyo imetolewa Mjini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini na Kaimu Makamu wa Rais wa Benki …

Soma zaidi »

KAMATI YA BUNGE YATOA MAONI KUHUSU MKATABA WA UMEME JUA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wametoa maoni mbalimbali kwa Wizara ya Nishati, kuhusu kuanzishwa kwa ushirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (ISA). Walitoa maoni hayo Dodoma, Novemba 12, 2019 wakiwa ni sehemu ya wadau wa sekta husika ili kuboresha Mkataba huo kabla haujawasilishwa …

Soma zaidi »

GESI TULIYONAYO LAZIMA ITUMIKE KUJENGA UCHUMI WA VIWANDA – DKT KALEMANI

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema mpango wa serikali wa miaka 30 wa matumizi sahihi ya rasilimali za gesi na mafuta, pamoja na mambo mengine, umelenga kuhakikisha gesi inatumika kujenga uchumi wa viwanda. Akizungumza katika ufunguzi wa Jukwaa la Tisa la Uziduaji, Novemba 6, mwaka huu jijini Dodoma, Dkt …

Soma zaidi »

HATUTAONGEZA MUDA – DKT KALEMANI

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amekataa maombi ya mkandarasi kampuni ya KEC International Ltd kutoka India, anayetekeleza mradi wa kupanua kituo cha kupoza umeme kilichopo Zuzu, mkoani Dodoma, kuongezewa miezi mitatu zaidi ili akamilishe kazi hiyo. Badala yake, Dkt Kalemani amemtaka Mkandarasi huyo kukamilisha kazi husika na kuikabidhi kabla …

Soma zaidi »

BODI YAWEKA KUSUDIO KUMFUTIA MKATABA MKANDARASI WA REA

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imeweka kusudio la kufuta mkataba mmojawapo wa mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Mtwara na sehemu ya Mkoa wa Tanga, ambaye ni muunganiko (JV) wa kampuni za Radi Services Ltd, Njarita Contractors Ltd & Aguila Contractors Ltd. Kusudio hilo liliwekwa bayana mbele ya waandishi …

Soma zaidi »

BODI YATOA TATHMINI KUHUSU UTEKELEZWAJI MIRADI YA UMEME VIJIJINI MOROGORO

Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Oktoba 25, mwaka huu ilikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Olesanare, taarifa ya tathmini kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo, baada ya ziara yao ya siku mbili. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Styden Rwebangila, …

Soma zaidi »

KASI YA WAKANDARASI MIRADI YA UMEME VIJIJINI TANGA YAIRIDHISHA BODI

Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB) imekiri kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa wakandarasi Derm Electrics (T) Ltd na JV Radi Services Ltd, Njarita Contractors Ltd & Aguila Contractors Ltd; wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Tanga. Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo, Oktoba 23, …

Soma zaidi »