Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baada ya mazungumzo yao Mhe. Rais Mstaafu Kikwete amesema wamekutana kwa utaratibu wa kawaida wa kusalimiana na kutakiana heri katika majukumu.
“Nimekuja kumsalimia nakumtakia kila la heri, anafanya kazi nzuri, aendelee tu kuchapa kazi na sisi tupo kwa namna yoyote ya kumpa nguvu, tupo tayari kumsaidia” amesema Mhe. Rais Mstaafu Kikwete.
https://youtu.be/030qK6mv0sk