Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa kukagua Mradi tanki la maji Bagamoyo litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.

TUNAFIKISHA MAJI SAFI VIJIJINI KWA 85% 2020 – MAMA SAMIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu ya tano imeendelea kutekeleza ahadi ya kusambaza maji mijini na vijijini ambapo mpaka ifikapo mwaka 2020 inategemea maji yatakuwa yamefika vijijini kwa asilimia 85% na mjini asilimia 90%.

MAKAMU WA RAIS A
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja  miundo mbinu ya maji itakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki la maji litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa tanki kubwa la mradi wa maji Bagamoyo lenye uwezo wa kubeba lita milioni 6 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku sita mkoani Pwani.

Ad

Makamu wa Rais ameipongeza Dawasa kwa kazi nzuri na amewataka wananchi kupitia kamati mbali mbali za maji kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji, miundo mbinu pamoja na mazingira yake.

“Wote tujitahidi kutunza vyanzo vya maji” alisema Makamu wa Rais

MTENDAJI MKUU WA DAWASA AKITOA MAELEKEZO KUTOKA KWA MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja ya miundo mbinu ya maji itakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki la maji litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.

Tenki hilo la Bagamoyo linatarajiwa kuhudumia wakazi wote wa mji wa Bagamoyo na vitongoji vyote vinavyozunguka mji huo.

Makamu wa Rais pia alipata nafasi ya kutembelea mradi wa uzalishaji na usambazaji vifaranga wa kampuni ya AKM Glitters na kuzungumza na wananchi waliojitokeza kwenye viwanja vya shule ya msingi Majengo.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais aliongozana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu na viongozi wengine wa Chama na Serikali.

MAKAMU WA RAIS AKIZUNGUMZA NA MTENDAJI MKUU WA DAWASA NA NAIBU WAZIRI WA MIFUNGO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa kukagua Mradi tanki la maji Bagamoyo litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.
Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *