Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ya vigae (tiles) moja alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang.

MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA MKOA WA PWANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa kuborsha barabra za Mkuranga kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati) wakati akikagua ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani kulia pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
  • Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo katika mkoa wa Pwani ambapo leo ametembelea Wilaya ya Mkuranga.
  • Katika ziara yake wilayani Mkuranga Makamu wa Rais alitembelea kiwanda cha kutengeneza Gypsum (Gypsum Board) cha Knauf kilichopo Mwanambaya, akiwa kiwandani hapo Makamu wa Rais aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuitambua nchi ya Tanzania kama nchi tajiri kwa malighafi za kutengenezea bidhaa mbalimbali pamoja na kuwa mlango mkubwa wa kuingilia Afrika Mashariki na Kusini
  • “Kwa Serikali kujua kwamba Tanzania ndio mlango mkubwa ndio maana tunachukua jitihada zote za kujenga miundombinu, miundombinu ya mabarabara, miundombinu ya reli, miundombinu ya usafiri wa anga ili tuweze kusafirisha kote Afrika na pengine nje ya Afrika” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea Gypsum Board kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Knauf kilichopo Mwanambaya Mkuranga Bw. Zachopolous Georgions.
  • Makamu wa Rais alikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami ya Mkuranga –Kisiju ambayo mpaka sasa kilometa 1.8 zimeshajengwa.
  • Makamu wa Rais alifanya ziara ya kustukiza kwenye mradi wa ujenzi wa ghala la Korosho la Serikali lililopo Kiparan’anda wilayani humo ambapo alionyeshwa kusikitishwa na Uongozi wa Bodi ya Korosho kwa kutozingatia maagizo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli lakini pia kutokuwa na uchungu wa pesa ya walipa kodi kwani ujenzi wa ghala hilo umesimama kwa muda mrefu na pesa zaidi ya bilioni moja imeshatumika katika eneo ambalo halifai kwa ujenzi wa ghala.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea Gypsum Board kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Knauf kilichopo Mwanambaya Mkuranga Bw. Zachopolous Georgions.
  • “Mheshimiwa Rais kapita hapa katoa maagizo na bado hayajatekelezwa mpaka leo bado lipo kwenye maji linaelea ghala hakuna kitu kinafanyika even a report kama Rais ulivyopita ulitoa maelezo haya tumefanya uchunguzi hii…uchunguzi wa ghala moja unachukua muda gani? Mwezi wa ngapi Rais alipita mpaka leo kwa hiyo inamaana mmepuuza maagizo ya Mheshimiwa Rais si ndio?” alihoji Makamu wa Rais wakati alipotembelea eneo hilo.
  • Makamu wa Rais aliendelea na ziara yake wilayani hapo kwa kutembelea kiwanda kikubwa cha Vigae (Tiles) cha Goodwill Ceramic Ltd ambapo aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwa moja ya kiwanda kinachotumia nishati ya gesi asili kuendesha shughuli zake pamoja na kutoa ajira zaidi ya 2000.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.
MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSSANI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ya vigae (tiles) moja alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang.
  • Wilaya ya Mkuranga ndio inaongoza mkoani Pwani kwa kuwa na viwanda 61 Vikubwa na Vidogo 429.
  • Katika Ziara hiyo Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega alitoa shukrani kwa Viongozi wakuu wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi nyingi ikiwa pamoja na ujenzi wa madaraja matano yaliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.
MAKAMU AKIW
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ya vigae (tiles) moja alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *