Rangi ya njano inawakilisha madini yote, sio dhahabu pekee yake – Rais Magufuli

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefuta mara moja maelekezo ya barua yenye kumbukumbu namba CHA.56/193/02/16 ya tarehe 23 Novemba, 2018 iliyoandikwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Baada ya kupokea maelekezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) kwenda kwa Wakuu wa Vyuo vya Ualimu, Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, Wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
  • Mhe. Rais Magufuli amesema barua hiyo yenye kichwa cha habari “MATUMIZI SAHIHI YA BENDERA, NEMBO NA WIMBO WA TAIFA” imetoa maelekezo ambayo yanaathiri uzalendo wa Watanzania na inaleta mkanganyiko wa tafsiri ya rangi na alama zilizomo katika bendera ya Taifa.

PHOTO-2018-12-14-18-25-25

 

  • “Hata mimi mwenyewe tangu nasoma shule hadi leo nafahamu kuwa Bendera ya Taifa ina rangi ya njano na sio rangi ya dhahabu, na rangi hiyo ya njano inawakilisha madini yote, sio dhahabu pekee yake.
  • Kwa hiyo nimeamua kuifuta barua hiyo na kama kuna mabadiliko basi ni lazima yafanyike kwa kuzingatia taratibu zote kwa kuwa jambo hili ni la Kitaifa, sio la mtu mmoja” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
  • Mhe. Rais Magufuli ameagiza Bendera, Nembo na Wimbo wa Taifa viendelee kutumika kama ilivyokuwa kabla ya kuandikwa kwa barua hiyo na ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwa wazalendo, kuipenda nchi yao na kuitangaza popote walipo ilimradi wanazingatia sheria na maslahi mapana ya Taifa.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SHERIA YA KODI YATOA MSAMAHA KWA MAPATO YASIYOZIDI MILIONI 4 KWA MWAKA

Na. Josephine Majura na Saidina Msangi, WFM, Dodoma Serikali imeeleza kuwa Sheria ya Kodi imetoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.